Home Makala Viongozi wa Afrika katika misukosuko

Viongozi wa Afrika katika misukosuko

304
0
SHARE

NA LEONARD MANG’OHA NA MITANDAO

Miongoni mwa habari zilizotawala vichwa vya habari katika vyombo vya habari kote duniani wiki hii ni pamoja na kufikishwa katika Mahakama ya Juu Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, utetezi dhidi ya tuhuma za rushwa na ufisadi zinazomkabili.

Tuhuma hizo zinadaiwa kutendwa na Zuma alipokuwa Rais wa Taifa hilo lenye uchumi imara zaidi barani Afrika, tuhuma ambazo yeye mwenyewe anadai kuwa ni njama zilizokuwa na lengo la kumwondoa katika ulimwengu wa siasa.

Zuma anakabiliwa na mashtaka dhidi ya rushwa, udanganyifu na kujitajirisha kinyume cha sheria kwa kufanya biashara ya mauzo ya silaha akiwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo katika miaka ya 1990, ambapo anashutumiwa kupokea rushwa kutoka katika kampuni moja ya Ufaransa ya Thales ili kuipa mkataba wa mauzo ya silaha uliokamilishwa mwaka 1999.

Zuma anatuhumiwa kushawishi baraza la mawaziri kumpatia mkataba huo wenye faida kubwa unaohusiha familia ya Gupta. 

vilevile kiongozi huyo anatuhumiwa kupokea rushwa katika kampuni inayoendeshwa na familia ya Watson.

Tuhuma hizo ndizo zilizotoa msukumo kwa Zuma kujiuzulu wadhifa wake wa urais Februari mwaka jana, na nafasi hiyo kuchukuliwa na Cyril Ramaphosa.

Zuma Anadai kuwa shirika la upelelezi la kigeni liko nyuma ya sakata hilo kwa lengo la kumtoa kumchafua na kwamba amejihakikishia kuwa anatuhumiwa yeye ni mfalme wa rushwa. Anadai kuwa licha ya kupewa majina ya watu waliopanga njama hizo ingawa hakufuatilia zaidi kuhusu sakata hilo.

Omary al Bashir

Hivi karibuni Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Sudan awamua kumhoji aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Omar al Bashir, kuhusu tuhuma za utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi, hatua ambayo imechukuliwa miezi michache baada ya kiongozi huyu mwa muda mrefu wa Taifa hilo kuondolewa madarakani.

Raia nchini humo waliandamana kulalamikia hali mbaya ya kiuchumi nchini humo ikiwamo kupanda maradufu kwa bei ya mkate kabla ya maandamano hayo kugeuka kuwa ya kupinga utawala wa Al Bashir wakimtaka ajiuzulu.

Kwa zaidi ya miaka 20 taifa hilo limekuwa katika migogoro ya wenyewe kwa wenyewe huku likiandamwa na matukio ya ugaidi jambo hali iliyosababisha Marekani kuliwekea vikwazo mbalimbali vikiwamo vya kiuchumi.

Joyce Banda

Kashifa ya ufisadi na rushwa dhidi ya Rais wa zamani wa Zambia, Joyce Banda, na hali mbaya ya uchumi katika taifa hilo ilimfanya kushindwa kuendelea na mhula wa pili wa urais katika Uchaguzi Mkuu wan chi hiyo uliyofanyika mwaka 2014.

Banda alijikuta katika kashfa mbaya ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka iliyofahamika kama Cashgate ambapo alituhumiwa kujilimbikizia mali akiwa Rais wa nchi hiyo.

Kutokana na sakata hilo polisi nchini humo walitoa kibali cha kukamatwa Banda baada ya kudai kuwa wamepata ushahidi wa kuamunika kuhusiana na sakata la uchotaji wa Dola za Marekani milioni 250 zaidi ya Sh bilioni 500, hali iliyoibua hisia kuwa huenda Rais huyo alitenda makosa makosa yabnayohusiana na matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji fedha.

Sakata hilo linatajwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo na jambo baya zaidi likimhusisha Rais wa nchi.

Mugabe

Akiwa na miaka 93 kiongozi mkongwe na mpigania uhuru wa Zimbabwe, Robert Mugabe, aliondolewa madarakani kama Rais wa nchi hiyo baada ya kuhudumu kwa miaka 38.

Baada ya kuondolewa kwake Mugabe na familia yake katika kizuizi cha nyumbani na huku jeshi la nchi hiyo likiahidi kuwachukuliwa hatua wale wanaomzunguka kiongozi.

Mugabe alijikuta matatani baada ya kumwondoa madarakani Makamu wake Emerson Mnangagwa na kumteua mkewe Grace kuchukua wadhifa huo.

Baada ya kuvuliwa urais chama chake cha ZANU-PF, kilimwondosha katika nafasi yake ya uenyekiti na kumteua Mnangagwa kukiongoza.

Kuondoshwa kwake madarakani ukawa mwisho wa utawala wake na kushuka kwa heshima na imani kubwa aliyoijenga katika Taifa hilo.

Bouteflika

Mapema mwanzoni mwa mwaka huu Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, alilazimika kujiuzulu wadhifa wake wa urais baada ya kuhudumu kwa miaka 20 kuanzia mwaka 1999.

Uamuzi huo wa kujiuzulu ulitokana na maandamano ya  wiki kadhaa ambapo Makundi ya vijana waliandamana kupinga utawala wake wakitaka mfumo mpya wa Serikali huku kukiwa na madai kuwa kiongozi huyo alikuwa anatumiwa na makundi vya kisiasa, biashara na maofisa wa jeshi.

Msukumo mwingine wa kumtaka kuondoka madarakani ulitoka kwa jeshi la nchi hiyo Jeshi la lililomtaka kiongozi huyo mwenye miaka 82 kutangaza kuwa hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya uongozi kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi kwa muda mrefu huku akiojitokeza hadharani mara chache.

Gaddafi

Kiongozi wa muda mrefu wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, aliondolewa madarakani kwa aibu na kisha kuuawa na vikosi vya Serikali ya Mpito ya nchi hiyo vilivyokuwa vikisaidiwa Jumuiya ya Kujihami (Nato ikiongozwa na Uingereza na Ufaransa na shinikizo la Marekani ambayo haikuingia moja kwa moja kijeshi katika Tifa hilo lenye utajiri wa mafuta barani Afrika.

Gaddafi aliondolewa madarakani baada ya maandamano ya muda mrefu ya kupinga utawala wake ambayo hata hivyo yanaelezwa kuwa ni matokeo ya chuki iliyopandikizwa kmiongoni mwa raia wan chi hiyo waliokuwa wakiishi barani ulaya na Marekani.

Mubarak/Morsi

Mwaka 2011 Misri ilishuhudia umwagikaji damu baada ya maandamano yaliyomaliza utawala wa miongo mitatu ya utawala wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak, kabla ya Taifa hilo kumpata Rais wake wa kwanza wa kidemokrasia marehemu.

Katika maandamano hayo zaidi ya watu 850 waliripotiwa kupoteza maisha jambo  ambalo lilisababisha Mubarak kuhukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kuchochea mauaji ya raia.

Marehemu Mohamed Morsi naye anaingia katika orodha ya viongozi waliondoka kwa aibu madarakani baada ya mwaka 2013, Taifa hilo likamwondoa madarakani na nafasi yake kuchukuliwa kwa muda kiongozi wa kijeshi Abdul Fatah Al-Sisi baada ya maandamano makubwa ya kuipinga Serikali yake.

Baade Mahakama nchini humo ilimhukumu kunyongwa baada ya kudaiwa kuhusika na kutoroka wafungwa wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011, kabla ya adhabu hiyo kubatilishwa mwaka 2016.

Morsi aliingia madarakani mwaka2012 lakini akaondolewa kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka mmoja baadae.