Home Habari VITA BIASHARA YA ‘UNGA’ IELEKEZWE VYUONI

VITA BIASHARA YA ‘UNGA’ IELEKEZWE VYUONI

877
0
SHARE

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

MOJAWAPO ya kundi ambalo limeathiriwa pakubwa na matumizi ya dawa za kulevya hata na kujihusisha na tabia chafu zikiwamo za mapenzi ya jinsia moja ni vijana. Kundi hilo kwa hakika kila kukicha linakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji nguvu ya ziada kuzishinda.

Vijana hawa wapo katika makundi mbalimbali, wapo ambao ni wasomi na hata wale waliopo mitaani, lakini Mwenyekiti wa Shirikisho la vyuo vikuu mkoani Tanga, Justus Tumaini, anasema hata vyuoni wapo watumiaji wa dawa za kulevya hivyo umefika wasaa wa kila kijana na Mtanzania kumfichua ili kutokomeza janga hilo.

Tumaini ambaye pia ni miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
mkoani Tanga ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Utumishi jijini
hapa.

Katika mazungumzo yake na RAI wiki hii, Mwenyekiti huyo anasema matumizi ya dawa za kulevya ni vita ambayo inapaswa kupiganwa nje na ndani, yaani kuanzia ngazi ya familia ili kuliokoa Taifa letu.

“Lazima vijana wapige vita masuala hayo kwa nguvu zote kwani wapo baadhi wanayatumia hivyo kupitia umoja wetu tunaweza kuona namna ya kupambana nao ili hali hiyo iweze kuondoka kwao.

Pamoja na mambo mengine akizungumzia utendaji wa Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, anasema utendaji wake ndani ya chama na Serikali umeakisi yale anayoyasema kutokana na namna anavyoweza kutatua na kusimamia kwa umakini masuala mbalimbali na kuhakikisha utulivu na umoja miongoni mwao unakuwepo.

Anaeleza mabadiliko ndani ya CCM ndiyo silaha kubwa ya kuweza kujipanga
hivyo suala hilo analiunga mkono kwani yatasaidia kuleta CCM mpya na Tanzania mpya.

“Suala la uwajibikaji kwenye jambo la kukiimarisha chama sidhani kama
linaendana na posho kwani pamoja na mabadiliko tunategemea waliobakia
wanaweza kutekeleza majukumu yao na kukifanya chama kuendelea kung’ara
zaidi,” anasema.

Aidha, akizungumzia baadhi ya watumishi wa umma kuogopa kufanya maamuzi katika utendaji wao kutokana na ‘tumbuatumbua’ inayoendelea kufanywa na wakuu wa mikoa na wilaya, mwenyekiti huyo anasisitiza watumishi hao wanastahili kuendelea kutumbuliwa kwa sababu asilimia kubwa walikuwa hawafanyi kazi kwa ufanisi.

“Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo, ndio maana Rais alipoingia madarakani
alianza na suala la ubadhirifu wa mali za umma kwa maana hiyo hivi
sasa kazi zitafanyika kitendo ambacho kiliweza kusababisha kuwepo kwa
watumishi hewa ambao walililetea Taifa hasara kubwa kwa kulipwa fedha
wasizostahili,” anasema.

Aidha, anatoa wito kwa vijana kuzingatia suala la uzalendo na utii kwa nchi yao jambo
ambalo linaweza kusaidia kujiandaa viongozi wa kesho wenye umakini na umadhubuti.

“Kwa Mkoa wa Tanga vipo vyuo 30 ambavyo kutokana na uimara wa uongozi
uliopo ndani ya shirikisho, nitahakikisha nawaunganisha ili kuwa
kitu kimoja kwa lengo la kukijenga chama na kukiendeleza,” anasema.

Aidha, pia wao kama shirikisho wamejipanga vizuri ili kushiriki
kwenye chaguzi zote za ndani ya siasa ili kuleta mabadiliko
ambayo yatakuwa na tija kubwa ndani ya chama hicho.

Anasema hivi sasa matarajio yake makubwa ni kukitumikia chama chake
kwa uzalendo ikiwemo kutumia elimu yake kwa matunda atakayoyapata
ikiwemo kuwa mwadilifu ili wengine waige mfano wao.

“Kama unavyojua unapokuwa kiongozi lazima uwe mzalendo na mwadilifu
na hiyo ndiyo sahihi ya kuweza kupata mafanikio lakini kufikia
matarajio yake ulionayo,” alisema.

Pamoja na mambo mengine, mwenyekiti huyo anatoa wito kwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kulipatia ufumbuzi haraka sakata la mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kitivo cha sheria ambaye hivi karibuni amefukuzwa chuoni hapo mara ya pili bila sababu za msingi.