Home kitaifa Wabunge: Serikali isitumie polisi kwenye uchaguzi

Wabunge: Serikali isitumie polisi kwenye uchaguzi

1054
0
SHARE

Maregesi Paul, Dodoma

Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma (CUF)ameitaka serikali isiwatumie askari polisi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika baadae mwaka huu.

 Amesema kwamba pamoja na kwamba polisi wanatakiwa kulinda amani, serikali imekuwa ikiwatumia kuharibu uchaguzi na kukipendelea Chama cha Mapinduzi (CCM) na hicho ni kinyume na sheria ya utawala bora ambayo inatambua mfumo wa vyama vingi nchini.

Nachuma pia ameitaka tume ya uchaguzi iwe huru wakati wa chaguzi za serikali za mitaa ili kila chama kishiriki kwa mujibu wa sheria.

 Wakati huo huo mbunge wa Moshi Mjini,Jafar Michael (CHADEMA) amewalaumu wakuu wa mikoa na wilaya kutumia madaraka yao vibaya kwa kuwanyanyasa wapinzani.

Katika hatua nyingine,Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) ameitaka serikali iunde tume kuchunguza malalamiko ya wananchi dhidi ya viongozi wao katika Wilaya ya Chemba.

Wabunge hao wameyasema hayo bungeni leo Aprili 11, walipokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Tamisemi, Utumishi na Utawala bora kwa mwaka wa fedha 2018/19.