Home Makala WAKENYA WAUNGA MKONO MGOMO WA MADAKTARI NAIROBI, KENYA

WAKENYA WAUNGA MKONO MGOMO WA MADAKTARI NAIROBI, KENYA

723
0
SHARE

Utafiti mpya nchini Kenya kuhusu mgomo wa madaktari unaendelea unaonyesha kwamba wananchi wengi wanawaunga mkono madaktari katika madai myao ya kutaka nyongeza ya mshahara ya asilimia 300.

Utafiti huo uliofanywa na taasisi ya Ipsos umeonyesha kwamba asilimia 51 ya wananchi wa Kenya wangependa kuona serikali inawalipa madaktari hao nyongeza yao ya mishaha kwa kiwango chote walichodai, wakati asilimia 27 wanataka madaktari hao walipwe nyongeza ambayo serikali imetamka kuwa na uwezo nayo kuwalipa.

Asilimia 56 ya hao wanaotaka serikali iwalipe madaktari nyongeza hiyo ni wafuasi wa muungano wa vyama vya upinzani chini ya mwamvuli wa CORD, wakati asilimia 31 ya wafuasi wa Muungano wa vyama vya Jubilee na asilimia 16 ya wafuasi wa CORD wamesema madaktari hao walipwe nyongeza yote wanayodai iwapo tu fedha zitakuwepo.

Ni asilimia 15 tu ya Wakenya ndiyo wanapinga madai ya madaktari kupewa nyongeza ya mishahara yao.

Mgomo wa madaktari nchini Kenya ulianza Desemba 5 mwaka jana na mazungumza ya kuwataka warejee kazini yalivunjika hata baada ya Waziri wa Kazi Phyllis Kandie kuingilia kati.

Wagonjwa kote nchini Kenya wameachwa bila huduma za afya kufuatia mgomo huo ambao umungwa mkono na wauguzi.

Hali hii imesababishwa kwa kutokuwepo maelewano kati ya serikali na chama cha madaktari nchini kuhusu serikali kuamuru madaktari walipwe na serikali kuu au serikali za majimbo.

Madaktari wanataka mishahara yao iendelee kulipwa na wizara ya afya kupitia serikali kuu.

Hospitali za umma ndizo zimeathirika zaidi kwani madaktari hawapo kabisa katika sehemu za kazi katika hospitali hizo ambapo huduma za afya za serikali sio ghali.

Katika hatua nyingine katika maamuzi yake Mahakama imesema mgomo huo wa madaktari ni kinyume na sheria wakati wiki iliyopita mahakama hiyo ilikuwa inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya viongozi wa vyama vya madaktari nchini humo (Kenya Medical Practitioners), na Mafamasuia na Waganga wa Meno (Pharmacists and Dentists’ Union) kwa kukataa kuwaambia wanachama wao kusitisha mgomo wao kama ilivyoamuliwa.

“Wakati wananchi wengi wa Kenya wanataka kuona madai yao ya nyongeza ya asilimia 300 yakitekelezwa, utafiti wa Ipsos uliofanywa kabla ya uamuzi wa mahakama uligundua kwamba Wakenya walikuwa wamegawanyika iwapo nyongeza hii ilipwe kwa wakati huu,”ilisomeka sehwmu ya utafiti.

Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (Central Organisation of Trade Union – COTU) Francis Atwoli amentaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati mazungumzo yaliyovunjika.

Hata hivyo akizungumza na gazeti moja nchini humo (The Standard), msemaji wa Rais Uhuru Kenyatta alikanusha madai tya kuvunjika kwa mazungumzo kwa kusema yalikuwa yakiendelea vizuri.

“Ni kweli tumekuwa na changamoto nyingi katika sekta hiyo (ya afya) kama vile uwiano wa idadi kati ya madaktari na wagonjwa…. Lakini kama ni mjadala kuhusu mgomo huu wa madaktari, suala lina linajadiliwa katika vikao sahihi,” alisema msemaji huyo wa Rais, Manoah Esipisu.