Home kitaifa Wakimbizi: Janga linalochagizwa na sera mbovu barani Afrika

Wakimbizi: Janga linalochagizwa na sera mbovu barani Afrika

512
0
SHARE
People gather at camp for internally displaced persons (IDP) set up amid old aircrafts near the airport in Bangui on December 29, 2013. Desperate Chadian refugees who fled chaos in the Central African Republic on Sunday recounted the horror they went through when they were attacked and threatened by angry mobs as the country became engulfed in sectarian violence. AFP PHOTO / MIGUEL MEDINA

HASSAN DAUDI NA MITANDAO

MWAKA jana, Afrika ilitajwa kuwa na idadi kubwa ya wakimbizi, ukilinganisha na mabara mengine, changamoto ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiisumbua AU (Umoja wa Afrika). Kwa kipindi cha miezi 12 pekee, Afrika ilikuwa na wakimbizi milioni 30.

Wakati ripoti hiyo inatoka, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ilitajwa kuwa kwenye hali mbaya zaidi, watu wake wapatao milioni 4.5 wakielezwa kuyakimbia makazi yao.  Mbali ya DRC, Somalia na Nigeria nazo zinatajwa kuwa na idadi kubwa ya wakimbizi.

“Ukitazama wengi wao (wakimbizi), wale waliokimbia makazi yao na kubaki ndani ya nchi yao ni wengi. Tatizo hili linapaswa kuandaliwa ajenda ya muda mrefu,” alisema Erol Yayboke, mkurugenzi wa Kituo cha Masuala ya Kimataifa chenye makao makuu yake mjini Washington (CSIS).

“… Kwa sasa, ni juu ya AU kwa sababu matatizo ya Afrika yanatakiwa kushughulikiwa na viongozi wa Afrika, hilo ndilo jambo la msingi,” alisema Yayboke, akiunga mkono mapendekezo ya ripoti ya UN iliyosisitiza: “Sheria zinatakiwa kuwapo ili kuwalinda wakimbizi Afrika. Bila shaka AU itafanyia kazi juhudi za kumaliza mizozo kati ya nchi, mfano mzuri ukiwa ni ule wa Ethiopia na Eritrea.”

Julai 12, mwaka huu, Meya wa majiji 10 kutoka sehemu mbalimbali duniani, walikutana chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa (UN), ikiwa ni moja kati ya hatua muhimu za kubaliana na changamoto hiyo ya wakimbizi.

Hatua hiyo ya kukutana ilitokana na ukubwa wa tatizo hilo ulimwenguni kote, ikikumbukwa kuwa tayari ripoti ya UN iliigusa Afrika Mashariki kwa kuonesha Uganda inashika nafasi ya tatu kwa kupokea wakimbizi wengi, ikitanguliwa na Pakistan na Uturuki.

Katika ripoti hiyo, Uganda ilitajwa kuwa kimbilio la wakimbizi wapatao 1,360,000, hivyo kuibua jibu kwamba hali ya kiusalama si ya kurudhisha barani Afrika. Ifahamike kwamba wakati DRC ikitajwa kuwa kwenye hali ngumu ya kiusalama, asilimia 30 ya wananchi wake 815,000 walikimbilia katika taifa hilo la Afrika Mashariki, Uganda.

Haisajaulika kwamba asilimia 10 waliingia Rwanda na asilimia tisa ni wale walijitosa Tanzania.  “Uganda ni nchi yenye ukarimu kwa wakimbizi, inawapa ardhi na kuwapa njia za kujitegemea,” ilieleza ripoti hiyo ya UN.

Lakini sasa, kama inavyoweza kuwa kwa mataifa mengine Afrika, bado Uganda si ya kujivunia linapokuja suala la wakimbizi, licha ya kutajwa kuwa ni ‘nchi yenye sera nzuri ya kuwapokea’.

Mfano, wakati ikielezwa kuwa kwenye kiwango kizuri cha kuwahakikishia uhuru wa kutembea bila usumbufu wakiwa nchini humo, makazi yanayoendana yanayoheshimu utu, haki ya kuajiriwa na kupata huduma za afya, bado ni tatizo linapokuja suala la elimu.

Unaweza kuliona hilo kirahisi kupitia sera ya elimu, ambao kwa kiasi kikubwa unamweka kando mkimbizi aliyekimbilia nchini humo. Ukweli ni kwamba bado uwezekano wa kuwafanya watoto wa wakimbizi wafurahie fursa sawa kielemu na wenzao ndani ya taifa hilo imebaki kuwa ndoto.

Mathalan, kwa mujibu wa Sera ya Elimu ya Maendeleo ya Uganda, katika hatua hiyo, watoto wanatakiwa kufundishwa kwa lugha zao za asili.

Wakati hali ikiwa hivyo, Ibara ya 32(1) ya Sheria ya Wakimbizi ya mwaka 2006 inakwenda kinyume cha matakwa hayo ya sera, ikieleza watoto wa wakimbizi wanatakiwa kupata haki sawa katika uwanja wa elimu, ikianzia ‘chekechea’.

Katika kile kinachoweza kuonekana wazi, huo ni mkanganyiko kwa sababu tu ni ngumu kwa watoto wa wakimbizi kufahamu lugha za makabila nchini Uganda hadi pale watakapokuwa wamekaa kwa muda mrefu nchini humo.

Ni kwa mazingira hayo basi, ili mtoto wa mkimbizi aweze kunufaika na elimu hiyo ya awali, basi atalazimika kurudia darasa, hali ambayo kwa mujibu wa utafiti, wengi wamekuwa wakiacha shule na kubaki kuishi kambini. Hapo unaweza kuona namna sera ya elimu ilivyo na utata.

Je, ni yapi madhara yake? Kwanza, idadi kubwa ya watoto wanaoshindwa kuendelea na shule hujikuta wakiingia katika magenge ya kihalifu, wengi wakiangukia kuwa wezi au makahaba. Lakini pia, hiyo imekuwa ikisababisha wakimbizi kuwa mzigo kwa jamii husika.

Ukiigeukia Uganda, tayari imeshaanza kukumbana na hali hiyo, ambapo wingi wa wakimbizi walioingia nchini humo wametajwa kuchagiza kundi la watoto wa mitaani au vijana wasio na ajira, sababu kubwa ikiwa ni kushindwa kuwapatia walau mafunzo ya ufundi.

Ni kwa muktadha huo, sit u Serikali ya Uganda na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosughulikia Wakimbizi (UNHCR), pia mataifa mengine barani humo, yanapaswa kuja na mpango wa kukabiliana na changamoto hiyo, kuhakikisha watoto wa wakikimbizi wanapatiwa mafunzo yenye tija kwa maisha yao katika siku za usoni.

Kupitia mkakati huo, si tu kuhakikisha wanapatiwa fursa ya kusoma, pia nchi husika inatengwa bajeti ya kutosha kuhakikisha wanaifurahia fursa ya elimu kama walivyo wenzao waliowakuta nchini humo. Pili, katika shule hizo, kunapaswa kuwapo kwa huduma za kisaikolojia kwa watoto hao.

Hiyo ni kwa sababu huenda msongo wa mawazo kutokana na matukio ya machafuko katika mataifa waliyotoka ukawafanya washindwe kufanya vizuri katika masomo au kuwaharibia maisha yao kwa ujumla.

Tatu, Wizara ya Elimu na Michezo zinapaswa kukaa chini na kuona zinavyoweza kutokomeza kikwazo cha lugha za kufundishia, mfano zile za makabila zinazotumika Uganda, ili watoto wa wakimbizi wanaopelekwa shuleni waweze kwenda sambamba na wenzao na kupata maaifa wanayopewa darasani.