Home Makala Wanasiasa waache wasomi watatue matatizo yao wenyewe

Wanasiasa waache wasomi watatue matatizo yao wenyewe

549
0
SHARE

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

SIASA za vyama vingi hapa nchini zimeonekana kushika kasi na kufanikiwa kupenya ndani vyuo vikuu. Ndani ya vyuo hivyo kumekuwapo na wanachama lukuki na viongozi ambao wamekuwa wavikiunga mkono vyama hivyo kwa namna mbalimbali.

Licha ya kusambaa kwa siasa vyuoni na kushika kasi kwa kiwango cha hali ya juu kumesababisha hata baadhi ya matukio makubwa ambayo yamekuwa yakijitokeza ikiwemo vurugu visizokuwa na tija.

Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Rai Alhamisi iliweza kuwatafuta
Marais wa Vyuo Vikuu hapa nchini kuelezea namna wanavyoona ushiriki wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu katika siasa.

Stanslaus Kadugalize ni Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wanafunzi wa
Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) anasema kwa mujibu wa sheria ya serikali ya mwaka 2005 inakataza vyuo vikuu kwa wanafunzi auserikali yake kuacha kujishughulisha kwenye masuala ya siasa.

Anasema kuwa licha ya hivyo lakini suala hilo linakatazwa ndani ya
maeneo ya chuoni lakini nje yake wanaweza kushiriki wao binafsi.

“Lakini serikali ya wanafunzi hairuhusu kujihusisha na masuala ya
siasa nje ya chuo kwani wanakuwa wamebeba mwamvuli wake, kwani mtu anaweza kwenda kupiga kampeni za udiwani na kusema kuwa yeye ni Rais wa Chuo hivyo hairuhusiwi kufanya hayo isipokuwa yeye mwenyewe kwa nafasi yake anaweza kufanya hivyo“Anasema.

Anaeleza kuwa siasa za vyama vya upinzani wanafunzi wana uhuru wa kushiriki nje ya eneo la chuoni kwani wanaweza kufanya hivyo kwani kwa mujibu wa sheri iliyopo hawaruhusiwi kujihusisha na masuala hayo ndani ya chuo.

Anasisitiza pia kuwa serikali ya wanafunzi hairuhusiwi kujishughulisha na masuala ya siasa ndani na nje ya chuoni kwa sababu ni serikali inayoongoza wanafunzi wenye matakwa mbalimbali ya vyama kwani linaweza kusababisha mpasuko ndani ya jamii inayohusika.

“Kama Juma Rais anakwenda kwenye masuala ya siasa lakini asitumike kwa mwamvuli wa chama husika kwani hali hiyo inaweza kusababisha mpasuko mkubwa kwao na jamii zinazowazunguka “Anasema.

Aidha anasema kuwa wasomi wa vyuo vikuu wanayohaki ya kujadili mwenendo wa kisiasa namna ulivyo hapa nchini kwa kutumia busara katika kuhakikisha jamii husika inaishi kwa amani na utulivu mkubwa.

Anaeleza kuwa msomi anaweza kujadili mwenendo huo wa hali ya kisiasa kwani anaruhusiwa kuonyesha taaluma yake na sio kushadadia anapokuwa kwenye masuala ya kisiasa kama msomi sio mwanasiasa.

“Kwa sababu wanaweza kusaidia kuelezea mustakabali wao bali sio kuingilia kwa ndani jambo ambalo linaweza kusababisha mipasuko ya kisiasa ndani ya jamii walizopo “Anasema.

Akizungumzia namna siasa zinavyoathiri vyuo vikuu anasema siasa hizo zina athari kubwa kwani vyuo vingi vikuu vyama vya siasa vimeingia kwa kasi ndani yao na hata chaguzi za serikali za wanafunzi vimekuwa vikitumika.

“Lakini pamoja na mambo yote hayo niwatake wanasiasa wawaache wasomi wana mambo yao ya kisomi na watuache sisi kama wasomi tutatue mambo yetu wenyewe “Anasema..

Sambamba na hilo alitoa wito kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini wasikubali kutumiwa na wanasiasa kwani wao wana fursa kubwa ya inayoweza kusaidia kutatua mambo kwa kutumia diplomasia kwa amani kuliko ilivyo kwa wanasiasa.

“Ukiangalia leo hii zipo athari kubwa kuingia kwenye siasa vyuo
vikuu kwani wanasiasa wanawatutumia kwa ajili ya kupata faida zao kwa kuweka ngome zao kwani hakuna mwanasiasa ambaye anaweza kumkataa msomi kwa kuwa ndio viongozi na wa vyama hivyo baadae.

Hali hiyo inasababisha wanasiasa hao kuendelea kuwatumia wanafunzi hao wasomi kwenye vyuo hivyo kwa kujenga ngome zao japo siasa ndani ya vyuo zinakatazwa kwa lengo la kuanzisha vurugu, kufanya maandamano”Anasema.

“Lakini pia wanasiasa watuache sisi kama wasomi wanafunzi
hatujashindwa kufanya mambo yetu ambayo yanaweza kutusaidia katika kufanikisha ustawi wa maendeleo hapa nchini na jamii kwa ujumla “Anasema.

Anaongeza kuwa makundi ya kisiasa yamekuwa kwenye mrengo wao kwa maslahi yao badala ya kuwasaidia wanatuacha sisi kama wasomi tutatue matatizo yetu wenyewe.

Naye kwa upande wake, Rais wa Serikali ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Tumaini Jijini Dar es Salaam(Tudaco), Josiah Sadock Busee anasema ushiriki wa serikali za wanafunzi kwenye masuala ya siasa ni jambo nzuri kama Taifa tunahitaji kuwa viongozi kwenye siasa za vyuo vikuu kwani wanapikwa  kwa ajili ya kuwawezesha baadae kulitumikia Taifa kwenye nyanya mbalimbali.

Anasema wanajifunza uongozi wanapokuwa kwenye vyuo vikuu kwa serikali imetoa nafasi ya wanafunzi wenye kuhitaji kuwa uongozi kujua namna ya kuweza kutatua matatizo yanayoikabili jamii.

“Taifa la leo linaundwa na vijana hivyo kupata uzoefu ni nafasi nzuri ya kwenda kujua nje lakini pia ina msaidia kwenda kuona namna ya kuyashughulia masuala mbalimbali ya kijamii,” anasema

Anaeleza siasa ya nje ni nzuri na wala sio mbaya kwani wanapata nafasi ya kupata uzoefu ambao unawawezesha kujua namna ya kuweza kuongoza jamii wakati wanapopewa fursa za uongozi.

Hata hivyo anaelezea athari zinazoweza kuwapata vijana wanaofanya siasa vyuoni kuwa ni wanakuwa wakakosa muda mwingi wa kusoma jamboambalo linasababisha kushusha viwango  vyao vya ufaulu.

“Kwani ni wazi wanafunzi wa vyuo vikuu wengine wanapokuwa wameingia kwenye masuala ya siasa wanakosa nafasi ya kusoma badala yake wanatumia muda mwingi kwenye mambo hayo kitendo ambacho kinachangia kushindwa kufanya vizuri kwani wanajisahau “Anasema.

Pamoja na hayo anasema kuwa kujihusisha huko kwa siasa kwenye vyuo kuna faida nyingi kuliko hasara endapo kiongozi husika anayepata nafasi ya kushiriki siasa ya nje kwa kuzingatia weledi na uadilifu mkubwa katika kuitumikia

“Sisi kama vijana tuna matumaini makubwa ya kulitumika Taifa lakini mbele sidhani kama kuna nafasi ya mtu kuingia kwenye siasa kwa mtazamo usiokuwa na mipango itakayoweza kutimiza malengo yake,” anasema.

Anasisitiza kuwa wapo watu wanaishi kwenye siasa ili kupata maslahi kama inapaswa pia sipingi wanafunzi hawatumiki lakini inategemea na mtu binafsi.

Akifafanua faida kupitia uongozi, Anasema wanapaswa kushiriki hasa siasa sio ya watu maana kupitia Tanzania itawaezesha kuweza kuongoza kwenye Taifa la kesho ambalo linaweza kuwa na viongozi makini na waledi.

“Sisi kama wanafunzi kupata nafasi ya kujihusisha kwenye siasa vyuoni sio baya kwani siasa inaweza kusaidia Taifa katika harakati za kujiletea maendeleo “Anasema.

Lakini pia anasema hakutakiwi ufujaji wa mali hivyo vijana wajitokeze kwa wingi kupata fursa ya kuongeza maeneo mbalimbali ikiwemo kuonyesha uzalendo, uadilifu na uwajibikaji utakaoweza kuwa chachu ya maendeleo.