Home Makala WANAWAKE NGUVU KAZI INAYOTUMIKA VISIVYO KISIASA

WANAWAKE NGUVU KAZI INAYOTUMIKA VISIVYO KISIASA

745
0
SHARE

NA SAFINA SARWATT, MOSHI


Unapozungumzia sekta zisizo rasmi nchini ni wazi kuwa unawazungumzia wanawake na vijana.

Kundi hili ni eneo ambalo limeonekana kama mpira wa kona kwani wanasiasa hulitumia sana katika masilahi yao ya kisiasa. Sekta zisizo rasmi ni mhimili mkubwa katika uchumi wa Tanzania lakini hautajwi wala kupewa umuhimu unaostahili

Zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wapo katika sekta hiyo, sekta rasmi ni asilimia isiyozidi 10 ambapo kitakwimu watanzania walioajiriwa rasmi

hawazidi 400,000, kwa hiyo utaona kuwa wavuja jasho ndio wengi hapa nchini, na ndio wanaoendesha maisha yetu kwa ujumla.

Katika makala hii tutaangalia kisheria juu ya haki za wanawake navijana ambao wanajishughulisha katika sekta zisizo rasmi, unaweza kujiuliza kwa nini wanawake na vijana?. Jibu ni sahihi kabisa.

Tanzania inakadiriwa kwamba wanawake hasa wa vijijini wanatoaasilimia 80 ya wafanyakazi katika eneo la kijiji na hivyo kutoa asilimia 60 ya chakula kinachozalishwa.

Ingawa wanawake ndiyo wazalishaji wakubwa wa mazao ya biashara, mazingira hayawaruhusu kumiliki mali zao hii ni kutokana na mfumo wetu ulivyo.

Wanawake hawana maamuzi juu ya masula ya uzazi, kwa mfano wanawake wengi hawana uwezo wa kuamua idadi ya watoto katika familia ingawa wao ndiyo wenye jukumu kubwa la kulea mtoto.

Si hivyo tu, vijana nao ndio wachakarikaji wakuu katika sekta zisizo rasmi kwa kuwa uhalisia hatuna ajira za kutosha na kuwafanya vijana wawe mtaani na ndio maana inawalazimu basi vijana na wanawake wakimbilie sekta hii isiyo rasmi.

Sasa tuangalie Dira ya Maendeleo ya 2025 ya Tanzania inayolengakuwapatia watu wake hali ya juu ya maisha, ili kufanikiwa katika kupata utawala bora wa kuheshimu sheria pamoja na kuendeleza uchumi imara na wa ushindani.

Dira hii inaendelea kufafanua kuwa ili kufanikiwa kuleta usawa wajinsia na kuwapa uwezo wanawake katika maeneo ya jamii, uchumi, uhusiano wa siasa na utamaduni lazima yatiliwe maanani.

Jinsia imewekewa kipaumbele katika masuala yote ya maendeleo ili kukuza uchumi wa Taifa, masuala ya siasa na utamaduni lazimayaangaliwe.

Jinsia ni mkondo mkuu ambao vipengele vyote vya maendeleo hupita ili kuimarisha uchumi wa Taifa, siasa na masuala ya jamii na utamaduni.

Kukosekana kwa ajira za kudumu hususani kwa vijana hapa nchi katika nyanja mbalimbali ni moja kati ya changamoto inayoikabili serikali kushindwa kujikwamua kutokana vijana ambao ndio nguvukazi kukosa ajira pamoja na kipato cha uhakika.

Kutokana na hali hiyo serikali pamoja na wadau wengine ambao tunaweza kusema ni wapenda maendeleo wamekuwa wakitumia njia mbali mbali za kuwainua vijana ili kuwezesha kuwa na kipato chakuaminika.

Moja ya njia ambazo vijana wamekuwa wakiingia na kupenda kuzitumia ni pamoja na ujasiliamali aidha ule mkubwa unaohitaji mitaji mikubwa au hata ule wa mtaji kidogo.

Kutokana na hali halisi ya kukua kwa teknolojia hapa nchini ni dhahiri kuwa uwezekano wa kuwapatia vijana ajira itakuwa vigumu kama ilivyokuwa zamani kutokana na kuwepo kwa teknolojia ya kurahisisha kazi zenyewwe

Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa mkoa ambayo imekumbwa na tatizo na tatizo hilo la ukosefu wa ajira kwa vijana za kudumu kwa vijana walio wengi hii ni kutokana na baadhi ya viwanda kufa.

Hata hivyo juhudi  zinafanywa na wadau mbambali kushirikiana na serikali ya kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana hao ambao ndio taifa la kesho

Lakini kwa matazamo wa jicho lingine vijana hawa kukosa ajira ndiomwanzo wa eneo umasiki kuanza kutumika  nikiwa na maana hadi hivi sasa hakuna mipango yoyote ya kuwainua vijana waliopo katika sekta zisizo rasmi

Kwa mfano leo hii tukiangalia mishahara ya maofisa wakubwa serikalini pamoja na wanasiasa utakuta ni mikubwa ila nguvu kazi ambayo ipo mitaani yaani vijana hawajajengewa uwezo Mkurugenzi wa shirika la Nguvu Kazi (Centre for Informal Sector Promotion) CISP, Abdalah Makange anasema kuwa serikali haoini wala haijafikiria jitahda katika kuwakomboa vijana walipo katika sekta zisizo rasmi na badala yake wamekuwa wakiwatumia kama miradi “Leo hii utakuta vijana waliopo katika sekta zisizo rasmi wakitumika kama vitega uchumi kwa wanasiasa kitua ambacho ni kosa wangetakiwa wawasaidie”anasema.

Katika azma ya kutafutia ufumbuzi tatizo hilo la ajira katika miaka ya ajira za kujiajiri vijana za zaidi ya laki 300,000 wamepatiwa ajira na shirika hilo la kiserikali lijulikanalo kama “nguvu kazi ”

Mkoa wa Kilimanjaro ambao una vijana zaidi ya million 1.5 kati yao wachache ndio wenye ajira na wengine hawana ajira kabisa ni wale walioko kwenye ajira isiyo rasmi yaani  kujiajiri wenyewe kwa maana nyingine ni wajasiliamali.

CISP  limewezesha vijana 500,000  katika kuwapatia mafunzo ya mazoezi kwa kuwafungulia miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwapatia maeneo ya kudumu yakufanyia miradi  ndongondongo kama vile kufyatua matofali, kusindika vyakula vya mboga mboga, kulima bustani za mbogamboga  na nyanya ufugaji wa kuku wa nyama ufundi wa sofa za magari mafundi gereje za magari ni kwajili ya kujipati fedha za kujikimu kimaisha

Shirika hilo liliazishwa mwaka 1990 ikiwa kama vikundi vya watu mbalimbali ambao hawana na ajira isiyo rasmi na kusajiliwa rasmi mwaka 1994 ikiwachukua vijana na kuwaweka katika hali ya kuwa kitu kimoja na  kuunda vikundi wakijifunza kila ufundi wa vitu mbalimbali .

Lengo ikiwa nikujua fani ya kila mmoja na kuwatenga kila wenye fani moja sehemu zao.

Kupata mafunzo ufundi biashara kujiunga katika vikundi kufuatana na fani zao za ufundi kuwaelekeza namna ya kupata mitaji ya biashara zao kupata maeneo ya kudumu ya kufanyia kazi zao ili kuweza kuinuka kiuchumi.

Hata hivyo, vikundi hivyo havikuwa na kiwango cha elimu ya mtu walikuwa wanatoa mafunzo ili kuongeza ufanisi kwa wale vijana wa mitaani na waliomaliza la saba hakuendelea na masomo ya kidato cha kwanza na

kuendelea na kuwaweka katika vikundi ya wale wenye ajira isiyo rasmi kwa kujiajiri wenywe na kuwa na sauti ya kwa pamoja

Serikali haijaweza kuonesha jitihada zake za kuwasaidia watu walio katika sekta zisizo rasmi na badala yake wamekuwa wakiwatumia kama miradi mara biashara zinapo imarika

Mkurungenzi wa shirika hilo la nguvu kazi Dk. Abdallah Makange, anaeleza kuwa ombwe hilo lisipozibika mapema ni muendelezo wa kuwa na vijana wasiokuwa na ajira.

Hata hivyo, anasema kuwa serikali pekee ndio inayotakiwa kukaa na kujipanga upya katika kutathimi maisha ha hatma ya vijana wasio kuwa na ajira rasmi ili kuweza kuwakwamua na hali ngumu a kimaisha inayozidi kila kukicha.

Wizara ya kazi, ajira na mendeleo ya vijana  ni bora ikakaa na kujipanga upya katika kuhakikisha inatafuta namna ya kuwasaidia vijana waliopo katika sekta zisizo rasmi tofauti na kuacha hali hii inaendelea kuongeza watu wsaiokuwa na ajira.