Home kitaifa Wanyamapori urithi wa asili Tanzania

Wanyamapori urithi wa asili Tanzania

3128
0
SHARE

JIMMY CHARLES,  ALIYEKUWA IRINGA

ZIPO nchi ulimwenguni ambazo hazina kabisa vivutio vya asili vya utalii, hali inayo walazimisha kutengeneza mazingira ili angalau kusaka uwiano.

Tanzaniani moja ya nchi chache duniani ambazo zimebarikiwa kuwa na maliasili nyingi katika kila pembe ya Taifa hili linalokadiriwa kuwa na zaidi ya watu milioni40.

Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) kwa kushirikiana na wadau wake USAID chini ya mradi wa PROTECT unadhihirisha ukweli wa hili, baada ya kufanya ziara maalum kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Ukweli ni kwamba hifadhi ya Ruaha ambayo ndio kubwa kuliko hifadhi zote nchiniimebarikiwa idadi kubwa ya wanyama pori.

Wanyamapor iwa Tanzania ni urithi wa asili na ni rasilimali yenye umuhimu mkubwa kitaifa na kimataifa.

Umuhimu wake umejikita katika

thamani ya kibiolojia ya spishi husika na mazingira ya asili yaliyopo.

Katika kulitambua hilo serikali ya awamu ya kwanza chini ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ilikuja na Azimio la Arusha ambalo hadi leo limekuwa likitumika kutoa mwongozo wa kuhifadhi wanyamapori katika.

Pamoja na historia yake ya muda mrefu katika kuhifadhi wanyamapori, Tanzania haikuwahi kuwa na sera kamilifu ya wanyamapori katikamuda wote huo.

Wanyamapori walikuwa wakilindwa na kutumiwa kwa kufuata maelekezo, kanuni na sheria zilizokuwa zikitumiwa na Idara ya Wanyamapori na asasi nyingine zilizokuwa zimepewa jukumu la kufanya hivyo.

Wakatiwa uhuru, mwaka 1961, idadi ya watu ilikuwakidogo takribani watu milioni nane,  idadi ambayo ilifanya pasiwepo na migongano yoyote ya matumizi ya ardhi, kutokana na kutokuwa na kasi kubwa ya maendeleo, tofauti na ilivyo sasa.

 Sehemuza ardhi ziliweza kutengwakwa urahisi kwa ajili ya kuhifadhi wanyamapori bila kuwaathiri watu walioshi karibu na maeneo hayo.

Sasa idadi ya watu imeongezeka sana na kuna maendeleo ya kisayansi na Kiteknolojia ambavyo husababisha uhitaji mkubwa wa ardhi.

Kwa kulizingatia hili, hapa ndipo inapoibuka hoja ya kuwapo kwa wadau kupaza sauti ili jamii ishiriki moja kwa moja katika kuwalinda na  kuwahifadhi pamoja na kutunza mazingira.

Uhai wa wanyamapori ni jambo linalotuhusu sana sote, viumbe hawa wa porini, wakiwa katika mapori wanamoishi si muhimu tu kwa ajili ya kutazamwa na Kuvutia,lakini pia ni sehemu ya maliasili yetu na pia ndio mustakabali wa maisha yetu ya baadaye.

Tusiposhiriki katika kuwalinda na kuwahifadhi wanyamapori ni wazi tunajiingiza katika hatari ya kuupoteza urithi wetu hasa kwa vizazi vijavyo.

Ipo haja kwa jamii  kutokuwa na utayari wakushiriki kwenye kuwaangamiza wanyama kwa kujali zaidi maslahi yao kuliko yaTaifa.

ADHABUNI KALI KWA MAJANGILI

Jamii inapaswa kukumbuka kuwa zipo sheria zinazosimamia wanyamapori pamoja na adhabu kali ambazo zinatolewa kwa mtu atakayewatendea isivyo halali wanyamapori.

Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 na kanuni za uhifadhi wa Wanyamapori (uwindaji wa kitalii) za mwaka 2010 zimefafanua sheria na adhabu zake.

Kifungu namba 19(1) kinaweka wazi kuwa mtu yeyote hataruhusiwa kushika au kumsumbua kwa makusudi mnyama yoyote ndani ya pori la hifadhi ya akiba ya wanyama pori pasipokuwa na ruhusa ya kimaandishi kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Naendapo atakutwa na hatia kwa mujibu wa kifungu cha 19 (2) (a) adhabu yake ni kifungo cha kati ya miaka mitano hadi 10 gerezani  na mahakama inaweza kuongeza faini kati yash. 500,000 hadi sh. milioni mbili.

Aidha kifungu cha 19 (2) (d) kinatoza faini ya sh. 200,000 hadi 500,000 au kifungocha kati ya mwezi mmoja ama miezi sita gerezani.

Kifungu cha 24(2) cha sheria hii kinaweka wazi kuwa mtu yeyote haruhusiwi kujeruhi au kusumbua jamii ya mnyama yoyote anayehifadhiwa  na adhabu yake ni faini ya kati y ash. 200,000hadi sh. milioni 10 kwa mujibu wa kifungu cha 116(2) (a) cha sheria hii.

Aidha kifungu namba 47(a), 4 (B)(i) vinakataza kuwinda bila leseni na hairuhusi wikuwinda mnyama au ndege zaidi ya waliyoidhinishwa katika leseni.

Adhabu ya mtu atakayekiuka sheria hii na kukutwa na hatia kwa mujibu wa kifungu cha 47(b) (aa) ni kwenda jela kwa muda wa miaka mitatu hadi 10 na mahakama inawezakutoa adhabu ya faini ambayo ni mara mbili ya thamani ya mnyama aliyewindwa.

Kiujumla vipo vifungu vingi ndani ya sheria hii ambavyo vyote vinatoa tahadhari sanjari na kuelekeza hukumu kwa mtu atakayewazuru wanyama.

Hata hivyo  Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka wazi kuwaipo kwenye hatua za mwisho za kuandaa sheria na kanuni za kuwezesha sekta ya wanyamapori na misitu inakuwa na mfumo wa jeshi usu badala ya uendeshaji wakiraia.

Waziri wa wizara hiyo, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la kuandaa sheria hiyo ni kukabiliana na ujangili, biashara haramu ya wanyamapori na mazao ya misitu.

“Serikali imedhamiria na imejipanga kuhakikisha inadhibiti matumizi haramu ya maliasili,ikiwamo uingizwaji wa mifugo kwenye maeneo yote ya hifadhi yanayohifadhiwa kisheria,” alisema Dk Kigwangalla.

Pia, alisema tafiti zinaonyesha hali ya hifadhi na mazingira Afrika inakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwamo za kisiasa, kiuchumi, ukuaji wa teknolojia,mabadiliko ya tabia nchi na ujangili.

Alisema Serikali inaendelea kupambana na changamoto hizo ili kuhakikisha wanyama wanakuwa salama ndani na nje ya maeneo ya hifadhi.