Home Habari Watumishi wa Mungu waja na uchumi ”CHOTARA ”

Watumishi wa Mungu waja na uchumi ”CHOTARA ”

1038
0
SHARE

NA LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

Hivi karibuni viongozi wa dini wametoa kitabu kinachoshauri kufanyika kwa mabadiliko ya mfumo wa uchumi nchini ili kuwa na uchumi jumuishi ambao utaharakisha maendeleo ya Taifa bila kumwacha mtu yeyote nyuma.

Mfumo huo unafahamika kama Uchumi wa soko jamii ama chotara ambao umeunganisha mfumo wa uchumi wa kijamaa na kibepari, umeandaliwa na wataalamu wa uchumi wa ndani chini ya Shirikisho la Viongozi wa Dini nchini linaloundwa na Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

Lengo mahususi la viongozi hao ni kusaidia kupata mfumo mzuri kutokana na mfumo wa sasa kutoeleweka kama ni wa kibepari au ujamaa. Mfumo huo unadaiwa kutumika katika nchi za Scandinavia ikiwamo Denmark, Norway, Iceland na Ujerumani na kuonesha mafanikio makubwa.

Waandaaji wa mfumo huu wanaeleza kupitia ripoti yao kuwa, baada ya kutathmini nadharia ya uchumi wa soko jamii kwa ujumla na kujua mafanikio ambayo nchi imefikia katika nyanja tofauti za kiuchumi na kijamii, ni dhahiri kuwa Taifa linahitaji kuweka upya mtazamo wake na fikra yake ya kiuchumi.

Serikali ya Tanzania ilianzisha mipango mikuu mitatu ili kuwa na maendeleo endelevu, mipango hiyo ni pamoja na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano na Mkakati Jumuishi wa Maendeleo ya Viwanda 2025.

Ili kuwa na utekelezaji wa mipango wenye mafanikio inaaminika kwamba ni vyema kila mwamanchi ashiriki na afaidike na matunda yatokanayo na ukuaji wa uchumi. Mfumo wa soko jamii unaonekana kuwa ni chaguo sahihi katika kujenga uchumi ambao ni imara, jumuishi na endelevu.

Mfumo huu wa uchumi soko jamii kwa hapa Tanzania unalenga kuwa na Taifa imara lenye maendeleo endelevu na taasisi zitakazojikita kuwezesha ukuaji na maendeleo ya kiuchumi yatakayowagusa watu wote.

Kwa sababu katika Dira ya Maenedeleo ya Taifa 2025, Tume ya Mipango ilikusudia kutengeneza miongozo mipya itakayozingatia uchumi wa soko baada ya sera za maendeleo kupata changamoto na kuhimiza uwapo wa dhana ya ubunifu, ujasiriamali na ushindani pamoja na uwekezaji wa kutosha katika maendeleo ya watu, mfumo huu pia unaongeza chachu na thamani katika dira ya maendeleo 2025.

Kutokana na uwezekano mdogo wa baadhi ya maeneo kufikiwa kikamilifu katika muda uliolengwa na dira ya maendeleo ikiwamo ubora wa maisha, jamii iliyoelimika, utawala bora na uchumi wa ushindani, mfumo huu unatoa mikakati na nguzo za kimaadili zitakazoboresha hali ya uchumi na maisha kwa baadae.

Waandaaji wa mfumo huu wanadai kuwa sera za sasa za umma zinakosa miongozo ya wazi, jumuishi na itikadi zitakazowekeza uwapo wa maendeleo kwa wote. Kwa hiyo mfumo huu ni matokeo ya tafakari ya pamoja itakayoleta ufumbuzi halisi wa changamoto mbalimbali kwa kuzingatia ushirikishwaji wa jamii.

Mfumo huu pia unapendekeza uwapo wa sera unaoainisha wajibu wa wadau wote muhimu katika kuunga mkono jitihada za kuleta maendeleo kwa kuzingatia mikakati ya muda mfupi na muda mrefu.

Katika mfumo huu shughuli zote za maendeleo ya nchi zinapaswa kuzingatia uwapo wa uchumi jumuishi kwa biashara huru na ushindani vinakuwa na uwiano mzuri unaosimamiwa na Serikali huku uwapo wa jamii na mazingira rafiki vikiwa ndiyo msingi wa uamzi.

Ufanisi  wa mfumo huu unategemea jinsi gani watekelezaji wake watakavyoelewa na kuhusianisha mfumo na shughuli za kibiashara katika ngazi zote kuanzia vijijini, Wilaya, Mikoa, Taifa na hata kimataifa

Hili linasababisha hitajio la watu kuwa na ujuzi na uelewa wa taarifa muhimu kuhusu shughuli za kiuchumi ili kukidhi mahitaji ya soko, ujuzi wa kitaalamu utakaowezesha kuwa na nguvu kazi yenye uwezo ambapo wanabainisha kuwa nguvu kazi iliyoelimika ni chanzo cha ubunifu na uwapo wa huduma bora.

Masuala mengine muhimu yanayoangaziwa kupitia mfumo huu ni pamoja na hekima hasa uwapo wa utawala bora kwa kutambua kuwa mfumo yenyewe ni wa kijamii hivyo binadamu ni chanzo au kitovu cha yote.

Pia unataka kuwapo uwajibikaji kwa watu wote kufanya kazi ili kufikia maendeleo, wafanya uamuzi kufanya uamuzi wa wenye athari chanya kwa uchumi, kuzingatia utawala wa sheria, haki ya mali binafsi na utaratibu wa kidemokrasia kama vile uchaguzi huru na haki kama moja ya njia ya kuondoa matendo miongoni mwa wadau.

Mambo mengine ni uzalendo kwa kuwa na watu wenye kulipenda na kujivunia Taifa lao, utajiri wa kitamaduni, jamii yenye amani na uwapo wa rasilimali ambapo wananchi wanapaswa kujengewa uwezo wa kuyafahamu mambo hayo.

Vilevile inashauriwa kujenga jumuiya inayotoa nafasi ya mshikamano, kufanya kazi pamoja na kusaidiana ili kufikia mafanikio. Hili linatajwa kuwa kuwa sehemu inayowawezesha watu kupata utambulisho wa pamoja kulingana na yanayowatofautisha au wanayofanana.

Pia msisitizo mkubwa unawekwa katika utu wa kibinadamu ambao unatajwa kuwa jambo muhimu katika kufanikisha maendeleo endelevu. Na wataalamu hawa wanaonesha kuwa ni vigumu nchi kudhani imeendelea kama wananchi wake hawawezi kuwa na rasilimali na mazingira rafiki kwa ustawi wa maisha. Kwa hiyo mfumo huu haupimi maendeleo kwa kuangalia kukua kukua kwa uchumi pekee pali pia kuruhusu watu kuboresha hali zao za maisha.

Masuala mengine yanayopewa uzito katika mfumo huu ni uadilifu ambapo wadau wote wanapaswa kuwa waaminifu ili kusimamia na kulinda wengine dhidi ya matumizi mabaya ya mamlaka, taasisi huru zisimamie ukusanyaji mapato na matumizi ya fedha na kutoathiriwa na wanasiasa wa wadau wengine.

Pia masuala kama vile tathmini, uwazi umoja na mshikamano ni miongoni mwa mambo yaliyopewa uzito ili kufikia ufanisi wa mfumo huo kwa maendeleo ya Taifa.

Mikakati

Wataalamu wameamua kuja na mfumo huu kutokana na hamasa walioipata kutoka katika mataifa yaliyofanikiwa kupitia mfumo wa Uchumi soko jamii lengo likiwa ni kusukuma maendeleo ya kiuchumi mbele.Katika kufikiwa maendeleo yenye usawa na hatimaye kupunguza umaskini kwa kiwango kikubwa.

Watalaamu hao wanadai kuwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, taarifa zinaonesha kuwa ukuaji wa uchumi pekee hautoshi kuondoa umaskini nchini.

Pia wanaonesha kuwa licha ya ukuaji wa uchumi wa asilimia saba mfumo wa sasa umeonesha kuwa siyo toshelevu kuweza kuleta maendeleo na kuboresha hali ya maisha katika jamii nzima na kwamba kukosekana kwa uwiano mzuri kati ya aliyenacho na asiyenacho na utofauti wa kitapo ngazi ya mikoa umeendelea kuongezeka.

Hivyo mfumo huu unawezesha uwapo wa biashara ya ushindani huru yenye ufanisi na inayoambatana na huduma za bina na  usalama zinazohahakikisha huduma huduma bora za mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wananchi na kupunguza changamoto za soko huru. Katika mfumo huu soko la ajira linakuwa lenye kuruhusu mabadiliko na kiwango cha mishahara kuendana na nguvu ya soko na kuhamasisha ajira mpya.

“Kiwango cha vijana wanaoingia katika soko la ajira Tanzania kinasababisha idadi kubwa ya watu wanaotafuta kazi, na hivyo kupelekea uwapo wa mishahara midogo na wimbi la na kiwango kikubwa cha wasio na ajira.

Ili kukabiliana na wimbi la umaskini kwa ufanisi soko la uchumi linapaswa kukidhi mahitaji ya wasio na ajira na kutoa sera za kijamii” inaeleza sehemu ya utafiti uliofanya na wataalamu hao.

Mipango na utaratibu

Mfumo huu wa uchumi unauwekaji wa malengo na kuhakikisha taasisi na wadau wanajua nafasi, majukumu na wajibu wao ambavyo vitakwenda pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana ili kufikia malengo yaliyowekwa. Pia kuwanhitajika kuwapo mfumo wa kisheria unaoaminika ili kuweka wazi aina ya shughuli ambazo zitafanywa na taasisi nyingine za umma na majumuko yapi yatafanywa na sekta ya umma.

Jambo jengine lilioangaziwa ni kuweka na kulina utaratibu unaolinda heshima bna utu wa Mtanzania, ambapo mikakati na mipango ya Serikali inapaswa kulenga kulinda watu wake dhidi ya uvunjifu wa haki za wafanyakazi au ajira kwa watoto. Pia kuhakikisha uhuru wa kukusanyika kama moja ya mambo muhimu katika jamii ya kidemokrasia na msingi wa wananchi kuanzisha, kubunina kuleta chachu ya mabadiliko katika uchumi.

Serikali pia itakuwa na jukumu la kutoa motisha zaidi kuliko kuingilia shughuli zote za kiuchumi, kuhakikisha upatikanaji wa huduma kama vile barabara, fursa za elimu msingi na huduma za afya zinazojitosheleza.

Mali binafsi

Katika mfumo huu sekta binafsi imepewa umuhimu mkubwa katika kuendesha shughuli za kiuchumi, ambapo mtu mmoja mmoja au kampuni anapaswa kupewa ulinzi wa kikatiba wa mali zao, na katika hili umiliki wa mali binafsi unabaki kuwa muhimu kwa wazazw kushiriki vizuri kwenye soko la ndani na la kimataifa. Kwa mujibu wa watatifi utaratibu huu unatoa motisha ya kuongeza kipato kupitia kazi za ni msingi wa ujasiriamali wenye ubunifu.

Taarifa ya Benki ya Dunia ya mwaka 2018 tanzania ilishika nafasi ya 142 kati wan chi 190 kwa urahisi wa kumiliki mali ambapo usajili wa mali unachukua wastani wa siku 67 na kugharimu kiasi kinachokaribia asilimia 5.2 ya thamani ya mali inayosajiliwa.

Utaratibu wa fedha

Hapa wanadai kuwa katika uchumi soko linahitaji sera za muda mrefu hasa zile zinazoleta uimara wa uchumi mkubwa na uhakika kwenye mfumo wa kuimarisha uchumi. Hivyo ni jambo la lazima ili kuwa na uwekezaji na uamuzi wa muda mrefu katika sojko la walaji.

Watafiti wanasisitiza ulinzi dhidi ya sera a fedha ambapo wanashauri uamuzi kuhusu fedha ukasimiwe kwa Benki Kuu. Hata hivyo wanakiri kuwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita Benki Kuu ya Tanzania imekuwa na uhuru zaidi, lakini imebaki kuwa na changamoto ya kuweza kuingiliwa na uamuzi wa kisiasa.

Ulini wa uchumi mkubwa

Miongoni mwa mambo yanayoshauriwa ni pamoja na Serikali kuwakikisha uwapo wa kiwango kidogo na imara cha mfumuko wa bei ambacho kinawakilisha uhitaji mkubwa wa bidhaa katika soko. Uwapo wa mfumuko mkubwa wa bei na usio imara unahatarisha ukuaji wa uchumi na sekta ya fedha.

Kwa mujibu wa vigezo vya Shirika la Fedha Duniani (IMF) Mfumuko wa bei ni vema uwe asilimia tatu. Kiwango kidogo cha mfumuko wa bei kinawakilisha uchumi imara na nkuonesha mwelekeo mzuri kama kiwango hicho hakitabadilika. Hata hivyo mabadiliko ya viwango vya riba kwa kipindi kirefu kunaweza kusababisha mabadiliko ya mfumuko wa bei.

Utaratibu wa biashara ma kuimarisha sekta binafsi

Katika huili Serikali inalo jukumu la kuweka mazingira rafiki ya ushindani wa kibiashara na kampuni za kibiashara zinapaswa kushindana kwa haki. Taratibu za kisheria kama vile mambo yanayohusu madeni, kamati za wafanyakazi, kodi na taarifa za wajibu zinapaswa kuwekwa wazi na kufahamika vizuri.

Kwa mujibu wa wataalamu hao uwapo wa biashara za wazawa katika soko la kitaifa na kimataifa kuna mchango mkubwa kwa mafanikio na uendelevu wa uchumi wan chi.

Kutokana na uchanga wa sekta binafsi nchi huku kampuni zinazomilikiwa na Watanznaia ambazo zinaweza kushiriki kikamilifu katika biasahara za kimataifa zikiwa bado ni chache nchi inapaswa kuhakikisha mazingira ya kibiashara yanahamasisha ustawi wa sekta binafsi ikiwa ni pamoja na mazingira mazuri katika michakato ya usajili wa biashara, utolewaji wa leseni, mifuko ya kodi na mambo mengine kadha wa kadha.

Mambo mengine muhimu yaliyogusiwa na wataalamu hao ni kuanzisha na kukuza biashara ndogo ndogo na za kati kwa kurahisisha uanzishwaji biashara hizo ili kuinuka kutoka nafasi ya 162 katika ya nchi 190 kama ambavyo ripoti ya Bemki ya Dunia ya mwaka 2018 inayoonesha. Kuhakikisha ushirikishwaji wa wadau wote katika kuandaa taratibu za kufanikisha biashara na ajira.

Serikali kuingilia katika matukio maalumu ili kuleta uwiano wa nguvu sokoni, kuhakikisha usalama wa biashara na katika mambo yenye maslahi kwa umma. Kukuza ushindani na masoko huria kwa Serikali kutodhibiti sekta zote jambo linalosababisha sekta binafsi kutozalisha kwa ufanisi. Kufuatilia masoko ilikuhakikisha kunakuwa na ushindani wa haki.

Jingine ni kutoa taarifa kwa uwazi kwa wadau wote jambo ambalo linahitaji kuwapo vyombo imara na huru vya habari na vinavyojitegemea kwa sababu uhuru wa vyombo hivyo una thamani katika kufikia maendeleo. Pia ni lazima Tanzania kama nchi kujenga uwezo wake kwa kutumia uhusiano wa kikanda na kimataifa ili kuimarisha maendeleo jumuishi ya uchumi.

Mengine ni pamoja na kuwa na utaratibu mzuri wa matumizi ya fedha, hapa Serikali inawajibika kuweka miongozo wa aina ya viwango vya kodi kwa wafanyabiashara na wananchi na kuwa na mamlaka moja inayokusanya kodi tofauti na sasa ambapo husimamiwa na mamlaka tatu ikiwamo mamlaka ya tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hili linapaswa kwenda sambamba na kurekebisha mfumo wa kodi utakaosaidia maendeleo jumuishi.

Katika eneo hili la kodi mambo mengine yaliyopewa uzito ni kupunguza tofauti za kiuchumi kwa kutoza kodi zenye uwiano ili kujenga mfumo wa kodi ambao wa muundo wake unaongeza usawa na haki kwa jamii, kubadili fikra ya kuweka motisha kwenye kodi, kurekebisha na kuufanya mfumo wa kodi kuwa endelevu na kuhakikisha ufanisi katika ukusanyaji kodi na mgawanyi wa mapato ya kodi kati ya mamlaka za Serikali Kuu na Serikli za Mitaa ili kuimarisha ugatuzi wa madaraka ngazi za chini na kuwezesha Serikali za mitaa kutoa huduma zaidi.

Pamoja na ni lazima kutoa ulinzi kwa jamii kupitia mfumo wa hifadhi ya jamii ulio wazi na rahisi ili kupunguza umaskini na kuondoa utofauti wa aliyenacho na asiyenacho. Ili kuhakikisha jambo hili linakuwa na tija kwa wote wanashauri Sheila ilazimishe kila mwananchi ajiunge na mfuko wa hifadhi ya jamii.

Elimu

Hata hivyo wataalamu hao wameliangazia suala ya elimu kama nyenzo na nguzo muhimu katika kufikia maendeleo endeleu na jumuishi, ambapo wanashauri kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora ya msingi kwa wote. Elimu ambayo itakuza vipaji na ushindani wa rasilimali watu na kwamba nchi inaweza kufungua mwanya wa vipaji vilivyojificha na ambavyo havijaibuliwa kwa kuwekeza kwenye mafunzo ya elimu.

Pia wanashauri kuboreshwa kwa mafunzo ya taasisi za elimu ya juu ili yaendane na mahitaji wa soko la ajira. Wanaeleza kuwa hii ni muhimu katika kuhakikisha wahitimu wa taasisi za elimu ya juu wanaajirika na kuwa na tija katika soko la ajira na kwamba tatizo kuu katika soko la ajira Tanzania ni upungufu wa watu wenye ujuzi.

Baadhi mambo mengine yaliyoshauriwa katika mfumo huo ni kutumia uwezo wa rasilimakli watu, kuunganisha na kuhusianisha malengo ya maendeleo katika masuala ya mazingira endelevu.

Sekta ya kilimo

Aidha wanasisitiza kuzingatiwa kwa sekta ya kilimo kutokana na umuhimu wake katika ajenda ya maendeleo ya uchumi wa Tanzania na kwamba maeneo mengi ya nchi kilimo bado ji nyenzo muhimu katika maisha watu hasa vijijini na kunachangia kwa sehemu kubwa ya uwa maisha wa wakulima.

Baadhi ya maeneo yaliyoshauriwa kuboreshwa ni pamoja na kupunguza utegemezi wa mvua kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kusaidia maendeleo ya kilimo kutokana na sekta hiyo kuwa duni na yenye matumizi madogo ya teknolojia, uhamasishaji wa nguvukazi na utoaji wa elimu vijijini ili kuongeza tija katika kilimo pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wakulima ili kuwapa ujuzi wa masuala ya masoko utakaowawezesha kujiamini.