Home Makala Zijue adhabu za kutumia mifuko ya plastiki

Zijue adhabu za kutumia mifuko ya plastiki

1151
0
SHARE

Na  Omari Kilwanda-Wakili

MTANZANIA mwenzangu unapaswa kuyafahamu makosa na adhabu zinazotolewa katika sheria zinazokataza matumizi ya mifuko ya plastiki.

Kimsingi kuna makosa makuu matano yaliyotajwa na kukatazwa ndani ya Sheria husika. 

Sheria hiyo Ndogo inajulikana kama The Environmental Management (Prohibition of Plastic Carrier Bags) Regulations, 2019. 

Sheria hii Ndogo imetungwa kwa Mujibu wa Kifungu Na. 230 (2) (f) cha Sheria inayojihusisha na Usimamizi wa Mazingira (The Environmental Management Act, Cap. 191).

A: MAKOSA

Kwa mujibu wa Kifungu/Kanuni Na. 8 Cha Sheria ya Kuzuia Matumizi ya Mifuko ya Plastiki ambayo ni  The Environmental Management (Prohibition of Plastic Carrier Bags) Regulations, 2019 kuna makosa matano ambayo ni;

(A). Kuzalisha na Kuagiza Mifuko ya Plastiki,  (Kifungu/Kanuni Na. 8 a );

(B). Kusafirisha nje ya nchi Mifuko ya Plastiki,  (Kifungu/Kanuni Na. 8 b );

(C). Kuhifadhi na Kusambaza Mifuko ya Plastiki, (Kifungu/Kanuni Na. 8 c );

(D). Kuuza Mifuko ya Plastiki, (Kifungu/Kanuni Na. 8 d ); 

(E). Kumiliki na Kutumia Mifuko ya Plastiki? (Kifungu/Kanuni Na. 8 e ).

B: ADHABU

Kwa kila kosa tajwa hapo juu, Sheria husika imetaja Adhabu yake. Hivyo basi kuna Adhabu aina tano kama ilivyo kwa Makosa husika. Kifungu/Kanuni Na. 8 cha Sheria tajwa hapo kilichotaja Makosa Matano ndicho hicho kimetaja Adhabu ya kila Kosa kama ifuatavyo;

(A). Adhabu kwa Wazalishaji na Waagizaji.

Kifungu/Kanuni Na. 8 (a) cha Sheria tajwa hapo juu, kinataja adhabu kwa mtu au watu hao kama ifuatavyo;

i. Faini isiyopungua  milioni 20 na isiyozidi Billioni moja (1),

ii. Kifungo kisichozidi miaka miwili,

iii. Au vyote Kifungo na faini tajwa hapo juu.

(B). Adhabu kwa wasafirishaji kwenda nje ya nchi.

Kifungu/Kanuni Na. 8 (b) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa mtu au watu hao kama ifuatavyo;

i. Faini isiyopungua milioni 5 na isiyozidi milioni 20,

ii. Kifungo kisichozidi miaka miwili,

iii. Au vyote, Kifungo na faini tajwa hapo juu.

(C). Adhabu kwa wanaohifadhi na wasambazaji

Kifungu/Kanuni Na. 8 (c) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja adhabu kwa mtu au watu hao kama ifuatavyo;

i. Faini isiyopungua  milioni 5 na isiyozidi milioni 50,

ii. Kifungo kisichozidi miaka 2,

iii.Au vyote Kifungo na faini tajwa hapo juu. 

(D). Adhabu kwa Wauuzaji

Kifungu/Kanuni Na. 8 (d) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;

i. Faini isiyopungua  laki 1 na isiyozidi laki 5*,

ii. Kifungo kisichozidi Miezi 3,

iii. Au vyote Kifungo na Faini tajwa hapo juu.

(E). Adhabu kwa Watumiaji na Wanaomiliki

Kifungu/Kanuni Na. 8 (e) cha Sheria tajwa hapo kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;

i. Faini isiyopungua Elfu 30 na isiyozidi Laki 2,

ii. Kifungo Kisichozidi  Siku 7,

iii. Au vyote Kifungo na Faini tajwa hapo.

Maoni ya Mhariri: Unaweza kuepukana na adhabu hizi, achana na matumizi ya mifuko ya nailoni, tumia mifuko ya karatasi inayotakiwa kutumika sasa, sheria acha sasa ili kuanzia Juni 1, mwaka huu uwe salama.