Home Makala Kimataifa Ala’a Salah ‘Shangazi’ aliyeweka alama ya kuanguka Rais Omar al Bashir

Ala’a Salah ‘Shangazi’ aliyeweka alama ya kuanguka Rais Omar al Bashir

3145
0
SHARE

Markus Mpangala

WANAWAKE na vijana. Watu wazima na watoto. Wote waliamua kwa kauli moja tu; Maandamano. Baada ya kutumia neno ‘maandamano’ mambo yakabadilika, ambapo mwihsoni mwa mwezi Machi waandamanaji wakaanza kuhubiri kuhusu Tharwa, yaani mapinduzi ya kumpindua Rais Omar al Bashir.

Waliimba, wakapiga gitaa, wakapiga kila aina ya vifaa vya muziki kusisitiza na kuburudishwa huku wakiwa na msimamo mmoja tu; kung’oa utawala wa miaka 30 wa Rais Omar al Bashiri.

Usuli wa maandamano ni unaanzia Januari mwaka 2018 wananchi wa Sudan walifungua rasmi ukurasa wa maandamano ya amani nchini humo kupinga kupanda bei za bidhaa nchini humo. Wengi waliingia mitaani kuandamana jijini Khartoum kupinga ongezeko la bei za Mikate.

Maandamano hayo yalipata msukumo baada ya watu wengine kuunga mkono hoja zilizochochea kuanzishwa kwake. Ilikuwa kama vile vita dhidi ya mamlaka. Mkate ukazua zogo, na ukatumika kama nyenzo ya kuelezea mfumuko wa bei ambao ulikuwa ‘unawazaba’ makofi kwa asilimia 70 kila mawio na machweo.

Vyama vya upinzani vikaona hiyo ni fursa yao ya kuungana na wananchi kupinga utawala uliokaa muda mrefu bila kutatua changamoto zinazowakabili. Wapinzani wakajumuika mitaani. Maandamano yakaota mizizi. Ilipofika Oktoba mwaka 2018 thamani ya fedha yao ikaporomoka. Uchumi ukapatwa na kwikwi, hali ya wananchi ikazidi kuwa mbaya. Ajira hakuna, ikazua zogo, vijana wakasema haiwezekani lazima rais awajibishwe.

Wasudan wakakasirishwa zaidi baada ya kusikia habari za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, Oamr al Bashir akipanga kugombea tena licha ya kuibuka upinzani mkubwa dhidi yake na sauti za kumtaka asigombee tena. Wanaharakati wakatumia mitandao ya kijamii, wakafanya kila mbinu kuhakikisha wananchi wanashiriki.

Desemba 19, 2018 hali ilikuwa ngumu zaidi. Kasi ya maandamano iliongezeka. Pumzika za watawala kuyakabili maandamano zilielekea kukoma, licha ya juhudi za Rais Bashir kufanya mabadiliko kwenye baraza lake la mawaziri. Maandamano yaliyoanzia  huko mjini Atbara, kisha kusambaa kwenye miji ya Port Sudan, Dongola na jijini Khartoum, huku maelfu ya wananchi wakichoma moto majengo ya chama tawala. 

Mwaka 2018 ukaisha, kiu ya wananchi wa Sudan haikukoma.  Mwaka 2019 ukaingia, bado wananchi wa Sudan walikuwa na kiu ileile ya mwaka uliopita. Hapo ndipo yakaibuka majabali mengine ya kuchangamsha maandamano hayo dhidi ya utawala wa Bashir. Wanadamanaji 800 walikamatwa na kuwekwa rumande pamoja na askari 19.

Muungano wa vyama vya wafanyakazi nao ukaingia mguu wake mitaani ambapo Januari 17 mwaka huu maandamano makubwa waliyofanya yaliongeza zogo kubwa dhidi ya serikali.

Pilika za mwezi Februari na Machi ziliwagusa wanawake wengi ambao walishuhudia wenzao wakiwa jela kwa sababu ya kuandamana huko. Licha ya serikali kutangaza kuwaachilia huru wanawake na waandamanaji wengine, wala wananchi hakukoma. Walizidisha maandamano na kupaza sauti zao.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Sudan imesema takribani watu 13 wamefariki dunia huku wengine 2,500 walikamatwa mjini Khartoum mwishoni mwa wiki iliyopita huku wengine 57 wakiwa wamejeruhiwa kutokana na maandamano hayo. Wimbi la waandamanaji lilizidi na ndipo askari wa Jeshi la Polisi waliagizwa kutotumia silaha zao dhidi ya watu wanaoandamana.

‘SHANGAZI’ ALAA SALAH

Hekaheka zote hizo ndizo zinamuibua Alaa Salah, msichana shupavu mwenye umri wa miaka 22 na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Sudan katika masomo ya uhandisi akawa kinara wa waandamanaji. Maandamano yalipamba moto, huku picha za video na mnato zikisambaa duniani kumwonyesha msichana huyo akiwa juu ya gari na kuwaongoza maelfu ya wananchi kuimba nyimbo za kupinga utawala wa Bashir.

Ala’a Salah amekuwa alama ya mapinduzi kwa harakati za kumuondoa Rais El Bashir madarakani. Alaa asema bunduki haiuwi watu isipokuwa ukimya ndio huuwa watu.  Amekuwa akiwapa waandamanaji nchini Sudan msukumo. Kutokana na juhud zake za uanaharakati, Ala’a Salah amekuwa maarufu hadi kwenye mitandao ya kijamii, vyombo vya habari vya kimataifa kama vile CNN,BBC na Al Jazeera kwa kuvitaja vichache. Picha yake ikachukuliwa alama ya mapinduzi dhidi ya Omar al Bashir. Ala’a amechukuliwa kama mwakilishi wa wanawake kwenye harakati za kudai haki na amani ya nchi hiyo, ambapo wanahistoria kubwa.

Lana Haroun, ndiye alipiga picha mnamo ya kwanza ambayo inatambulika kama alama ya mapinduzi dhidi ya Bashir nchini Sudan. Akizungumza na CNN, Lana Haroun alisema, “Alikuwa anawakilisha wasichana na wanawake wa Sudan, amekuwa chachu kwa pande zote, kuwa wanawake na wanaume wanaweza kushirikiana katika jambo hili,”

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Sudan, Ahmed Kaballo, mwenye makazi yake nchini Uingereza aliliambia gazeti la The Independent juzi, “Nilipoona picha ya msichana huyo, nilitabasamu, na nina uhakika kila mmoja inaweza kumfurahisha. Ingawa baba yangu anashikiliwa rumande kwa miaka miwili bila kufunguliwa kesi mahakamani, daima alizungumzia umahiri na nafasi kubwa ya wanawake wa Sudan walivyoshiriki katika historia ya ukombozi wa nchi hiyo,”

KANDAKA

Kana kwamba haitoshi, wananchi wenzake wameamua kumpa jina la heshima binti huyo la Kandaka ambalo ni ishara ya wanawake na wanaume kupambana dhidi ya ukoloni wa Uingereza nchini Sudan. Vazi alilovaa linahusishwa na yale ya wapigania uhuru na haki za wananchi nchini Sudan kati ya miaka 1960 hadi 1980. Vazi hilo linatajwa kuwa maalumu kuvaliwa kwenye maandamano mitaani kupinga utawala wa mabavu.

“Wananchi wa Sudan kila mahali, mwanamke anayeshiriki na kuongoza maandamano wanamwita Kandaka, likiwa ni jina la heshima walilokuwa wakipewa Malkia wa Nubia katika kipindi cha Sudan ya kale. Ni kama zawadi kutokana na urithi wa kihistoria kuonyesha nguvu za wanawake katika mapambano,” alisema mchambuzi huyo.

Aliongeza kuwa, “picha ya Ala’a Salah inawakilisha nafasi ya wanawake wa Sudan katika matukio ya mapambano ya kutafuta haki na matumaini kwa wananchi wote.

THAWRA

Kwenye picha ya video, Ala’a Salah anaonekana akiimba kwa furaha na kuhawahamaisha maelfu ya waandamanaji wenzake kushiriki na kusonga mbele hadi kumng’oa Omar al Bashir. Maneno aliyokuwa akitamka ni ‘Thawra”, ambalo lina maana ya mapinduzi.

Ala’a aliimba na kucheza, aliwakaribisha wananchi wenzake, alihamasisha kutositisha maandamano na kuhakikisha wanapinga utawala wa mabavu,uonevu na usio na misingi ya haki. Wimbo huo umetafsiriwa kwa lugha ya kiingereza, ambapo kwa Kiswahili unasomeka kama ifuatavyo;

‘Oh Mama nisamehe, Ahadi yangu sikutimiza,

Sababu hotuba imekatazwa, Na viongozi wahuni,

Oh Mama damu iimekuwa juisi yao, wakati nchi inazidi kuchemshwa

Wakati hawa askari, wamechafua sura ya uislamu

Wanatuletea makabati yao, yaliyojaa silaha

Hofu, Oh ni hofu, hakuna sababu ya kuhofia,

Kila kona kuna mizigo ya damu, magereza yafunguliwe zaidi

Kinachotuua si risasi, ukimya ni adui yetu