Home Habari ZIMBABWE YA MUGABE, ROMA MKATOLIKI!

ZIMBABWE YA MUGABE, ROMA MKATOLIKI!

5032
0
SHARE

“…Maslahi ya Taifa! Taifa Kwanza! Uzalendo! Uhuru wa Taifa, Kulinda Usalama wa Taifa letu!”

Maneno yote hayo kwa sasa yanatumiwa kwa malengo ya kulinda vyeo na ukuu wa watu, kunyanyasa na kusweka watu rumande kwa kiburi, kibabe na bila sababu.

Maneno hayo hayo ndiyo ameyatumia Robert Mugabe kuifikisha Zimbabwe mahali ilipo. Zimbabwe ya leo haina sarafu, sarafu yake imekufa, uchumi wake umekufa. Zimbabwe inatumia Dola ya Marekani na Bondi za Benki kufanya manunuzi. Zimbabwe imerudi kwenye “Barter Trade.”

Na Zimbabwe inaamini kuwa Mugabe anaifikisha hapo ilipo ili kulinda maslahi ya Taifa! Taifa Kwanza! Uzalendo! Uhuru wa Taifa na Usalama wa Taifa.

Laiti kama Wazimbabwe wangelizinduka, adui yao nambari moja, ni Mugabe mwenyewe. Ambaye yuko tayari kuwaaminisha kuwa Wamarekani na Waingereza ni watu hatari sana, and yet, mkewe (Grace Mugabe) kila siku anashinda Marekani na London, kufanya manunuzi ya mamilioni ya dola kwa kodi zao.

“Hii ni Zimbabwe ya Roma Mkatoliki”, nazungumzia Zimbabwe ile ya Zimbabwe, na ile nyingine ya Afrika Mashariki ambayo hata kama unajidai huijui, ukweli ni kuwa unaijua vizuri tu, na namba unaisoma!”

Julius Mtatiro