Home Uchambuzi MAADUI WA TUNDU LISU NI KINA NANI?

MAADUI WA TUNDU LISU NI KINA NANI?

10926
0
SHARE

Siasa za nchi yetu zimepevuka na kupata sura mpya. Kama taifa kiongozi kwenye maswala ya kiusalama tumepata doa kubwa sana.

Tanzania hatukuwahi kuzoea milio ya Bunduki, Hatukuwahi kuviziana na kuanza kuwindana kama wanyama.

Dalili za matukio haya zilishaanza kujionyesha muda mrefu sana. Si mara moja tulimsikia Lisu akisema kuna watu wanfuatilia na gari.

Cha kushangaza hakuna ulinzi wowote aliowekewa na chama chake au Serikali. Nani atakayetuelewa kama Lisu angelipoteza maisha?

Machafuko yakijitokeza tumaweza kujilaumu? Katika kipindi kama hichi ambacho umaarufu wa Lisu umeongezeka Lolote linaweza kutokea hivyo alipaswa kuwekewa Ulinzi maalumu.

Kosa kubwa ninaloliona kwa serikali ni kutokumlinda Lisu. Kwa kuwa Lisu amekuwa akisuguana na Serikali siku za karibuni maadui zake wanaweza kumdhuru ili ionekane kuwa ni serikali imefanya jambo kama hilo.

Kosa kubwa kwa chama chake ni kutokumpatia Lisu ulinzi wa kutosha katika kipindi hiki anacholalamika kuwa anafuatiliwa na watu asiowajua. Swali la kujiuliza kwa kazi anazozifanya Lisu chama chake hakikuwahi kufikiria kumwongezea Lisu usalama wake?

Ambacho watu wengi hawataki kujiuliza ni kwamba ni nani anayeweza kuwa adui wa Lisu hapa nchini? Nafikiri jambo la msingi lilikuwa ni kuorodhesha maadui zake kwanza na kuanza kutafuta nani anayehusuka kati ya hao maadui.

Tukianza kunyooshe watu flani kuwa ndio wanaohusika moja kwa moja tutampoteza aliyehusika kweli.

Kitu kingine ambacho watu hawakijui ni kwamba maadui pia wa Rais Magufuli wanaweza pia kuhusika na shambulio hilo ili kumchafulia kwa kuwa watu watahusisha ukosoaji wa Lisu na dots za kukamatwa kwake kila mara na jambo lililomtokea.

Wanaomuita rais Magufuli Dikteta pia wanaweza kufanya chochote kujustfy wanachokiimba. Tupo gizani sana Mungu atupe mwanga wa kuyaona haya.

Na hapa ndipo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinatakiwa vilifanyie eneo hilo kazi ya ziada.

Njia pekee ya kuondoa sintofahamu hii ni polisi wetu na vyombo vingine vya kiuchunguzi kuja na ripoti kamili ya ni nani anayehusika na jambo hili.

Utakuwa huna akili kama hutakuwa na assumptions hizi ukaanza kuropoka kwa kuwanyooshea watu vidole.

#Mungu amponye haraka Tundu Lisu.

Thadei Ole Mushi