Home Makala Kimataifa Migogoro ya tembo, binadamu yaitesa Thailand

Migogoro ya tembo, binadamu yaitesa Thailand

2604
0
SHARE
Meneja Mradi wa Shirika la Uhifadhi Mazingira Duniani (WWF) nchini Thailand, Nares Suaturian akielezea jambo msafara wa waandishi wa habari waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Kui Buri nchini Thailand.

NA MWANDISHI WETU, ALIYEKUWA BANKOK

KUKOSEKANA kwa mahitaji muhimu ya wanyamapori ndani ya hifadhi ya Taifa ya Kui Buri nchini Thailand kunatajwa kusababisha mgogoro kati yao na binadamu. Shirika la Uhifadhi Mazingira Duniani (WWF) nchini humo limewaambia waandishi wa habari za mazingira kutoka nchini Tanzania waliopo kwenye programu maalumu iliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la RTI chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAIDProtect) kuwa mgogoro mkubwa unawahusisha binadamu na tembo, ambao wanalazimika kwenda kwenye makazi ya watu kusaka maji na chakula.

Imeelezwa kuwa nchi hiyo kwa sasa inakadiriwa kuwa na tembo zaidi ya 3,000, huku kiasi cha tembo 300 wakipatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Kui Buri.

Idadi hiyo ya tembo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kui Buri inatajwa kuwa kubwa kuliko tembo waliopo kwenye hifadhi nyingine nchini humo. Meneja Mradi wa Shirika la Uhifadhi Mazingira Duniani (WWF) nchini Thailand, Nares Suaturian amebainisha kuwa wanafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo.

Suaturian alisema wameamua kutega kamera zenye uwezo wa kunasa matukio yanayofanywa na wanyama hasa tembo ndani ya hifadhi kwa muda wote wa mchana na usiku. Taarifa zinazokusanywa kupitia kamera hizo, hupokelewa kwenye kituo maalum cha kupokea taarifa na kufanyiwa kazi kwa haraka. Alisema kamera hizo zimefungwa kwa ustadi mkubwa juu ya miti mikubwa iliyo karibu na mishoroba ya tembo.

Suaturian alisema ingawa hawajafanikiwa kumaliza changamoto hiyo, lakini kuna mafanikio kidogo yamepatikana baada ya kufunga kamera hizo katika mishoroba 25. “Kazi kubwa ya kamera hizi ni kuwafuatilia tembo, tunaamini wapo tembo zaidi 237 huku tembo wanawake wakiwa zaidi ya 168.

“Tunachokifanya ni kuhakikisha wanyama hawa hawaingii kwenye maeneo ya makazi na kwenda kuharibu mazao, hatujalimaliza jambo hili, lakini angalau kuna mafanikio kidogo na hatujakata tamaa bado tunasaka njia zaidi za kuhakikisha tunamazaliza kabisa jambo hili.” “Kamera tulizofunga ni za

kwa mahitaji muhimu ya wanyamapori ndani ya hifadhi ya Taifa ya Kui Buri nchini Thailand kunatajwa kusababisha mgogoro kati yao na binadamu.

Shirika la Uhifadhi Mazingira Duniani (WWF) nchini humo limewaambia waandishi wa habari za mazingira kutoka nchini Tanzania waliopo kwenye programu maalumu iliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la RTI chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAIDProtect) kuwa mgogoro mkubwa unawahusisha binadamu na tembo, ambao wanalazimika kwenda kwenye makazi ya watu kusaka maji na chakula. Imeelezwa kuwa nchi hiyo kwa sasa inakadiriwa kuwa na tembo zaidi ya 3,000, huku kiasi cha tembo 300 wakipatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Kui Buri.

Idadi hiyo ya tembo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kui Buri inatajwa kuwa kubwa kuliko tembo waliopo kwenye hifadhi nyingine nchini humo. Meneja Mradi wa Shirika la Uhifadhi Mazingira Duniani (WWF) nchini Thailand, Nares Suaturian amebainisha kuwa wanafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo.

Suaturian alisema wameamua kutega kamera zenye uwezo wa kunasa matukio yanayofanywa na wanyama hasa tembo ndani ya hifadhi kwa muda wote wa mchana na usiku. Taarifa zinazokusanywa kupitia kamera hizo, hupokelewa kwenye kituo maalum cha kupokea taarifa na kufanyiwa kazi kwa haraka. Alisema kamera hizo zimefungwa kwa ustadi mkubwa juu ya miti mikubwa iliyo karibu na mishoroba ya tembo.

Suaturian alisema ingawa hawajafanikiwa kumaliza changamoto hiyo, lakini kuna mafanikio kidogo yamepatikana baada ya kufunga kamera hizo katika mishoroba 25.

“Kazi kubwa ya kamera hizi ni kuwafuatilia tembo, tunaamini wapo tembo zaidi 237 huku tembo wanawake wakiwa zaidi ya 168. “Tunachokifanya ni kuhakikisha wanyama hawa hawaingii kwenye maeneo ya makazi na kwenda kuharibu mazao, hatujalimaliza jambo hili, lakini angalau kuna mafanikio kidogo na hatujakata tamaa bado tunasaka njia zaidi za kuhakikisha tunamazaliza kabisa jambo hili.”

“Kamera tulizofunga ni zawa mahitaji muhimu ya wanyamapori ndani ya hifadhi ya Taifa ya Kui Buri nchini Thailand kunatajwa kusababisha mgogoro kati yao na binadamu.

Shirika la Uhifadhi Mazingira Duniani (WWF) nchini humo limewaambia waandishi wa habari za mazingira kutoka nchini Tanzania waliopo kwenye programu maalumu iliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la RTI chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAIDProtect) kuwa mgogoro mkubwa unawahusisha binadamu na tembo, ambao wanalazimika kwenda kwenye makazi ya watu kusaka maji na chakula. Imeelezwa kuwa nchi hiyo kwa sasa inakadiriwa kuwa na tembo zaidi ya 3,000, huku kiasi cha tembo 300 wakipatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Kui Buri.

Idadi hiyo ya tembo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kui Buri inatajwa kuwa kubwa kuliko tembo waliopo kwenye hifadhi nyingine nchini humo.

Meneja Mradi wa Shirika la Uhifadhi Mazingira Duniani (WWF) nchini Thailand, Nares Suaturian amebainisha kuwa wanafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo.

Suaturian alisema wameamua kutega kamera zenye uwezo wa kunasa matukio yanayofanywa na wanyama hasa tembo ndani ya hifadhi kwa muda wote wa mchana na usiku.

Taarifa zinazokusanywa kupitia kamera hizo, hupokelewa kwenye kituo maalum cha kupokea taarifa na kufanyiwa kazi kwa haraka.

Alisema kamera hizo zimefungwa kwa ustadi mkubwa juu ya miti mikubwa iliyo karibu na mishoroba ya tembo. Suaturian alisema ingawa hawajafanikiwa kumaliza changamoto hiyo, lakini kuna mafanikio kidogo yamepatikana baada ya kufunga kamera hizo katika mishoroba 25.

“Kazi kubwa ya kamera hizi ni kuwafuatilia tembo, tunaamini wapo tembo zaidi 237 huku tembo wanawake wakiwa zaidi ya 168.

“Tunachokifanya ni kuhakikisha wanyama hawa hawaingii kwenye maeneo ya makazi na kwenda kuharibu mazao, hatujalimaliza jambo hili, lakini angalau kuna mafanikio kidogo na hatujakata tamaa bado tunasaka njia zaidi za kuhakikisha tunamazaliza kabisa jambo hili.” “Kamera tulizofunga ni za

kisasa, zinauwezo mkubwa wa kufuatilia matukio ya wanyama kwa muda wote hatua inayowasaidia askari wa wanyamapori kujua ni eneo gani tembo wamevuka mipaka na kuingia kwenye makazi ya watu.

“Taarifa zikishapatikana, haraka askari huchukua hatua ya kwenda kuwarudisha wanyama hao kabla hawajasababisha hasara na madhara kwa wanakijiji,” alisisitiza Nares Aliongeza kuwa kamera inaponasa tukio haraka hutuma picha hizo kwenye kituo maalumu kilichoanzishwa kwa ajili ya kufanya mawasiliano kati ya askari wa wanyamapori waliopo kituoni na wale waliopo doria ili kuhakikisha wanyama hao hawaharibu mashamba ambayo yapo pembezoni mwa Hifadhi ya Kui Buri.

“Tangu tumeanza kutumia mpango huu tumeshapata picha 300 na niseme tu kabla ya mpango huu, uharibifu ulikuwa mkubwa tofauti na hali ilivyo sasa kwa maana matukio ya uharibifu yaliyorekodiwa yalikuwa ni zaidi ya 195 tofauti na sasa.” Alisema njia inayotumika kuwarejesha tembo hao hifadhini ni kuwapigia kelele na makofi na si kuwachapa ama kuwajeruhi kwa namna yoyote ile. “Kmaera zimefungwa kwa umbali wa mita 100 kutoka eneo la wanakijiji, hazina usumbufu kwa binadamu wala kwa tembo na si rahisi kuonekana.

“Migororo hiyo bado ni changamoto, tunajitahidi kutafuta namna ya kuikabili, huu utegaji wa kamera unatupa matumaini, lakini pia bado tunaumiza vichwa ili kupata namna bora zaidi ya kukabiliana na suala hili.

“Miongoni mwa mbinu tunazozifikiria ni kuhakikisha tembo wanapata mahitaji yao muhimu kama vile maji na chakula, hivi ndivyo vitu tunavyoamini kuwa vinawalazimisha kutoka hifadhini.

Mkuu wa Hifadhi ya Kui Buri, Tassanes Petchkong alisema kuwa pamoja na kuwapo kwa changamoto hiyo, lakini yapo mafanikio ambayo wanajivunia juu ya hifadhi hiyo yenye ukubwa wa kilomita za mraba 969.

Petchkong, alisema hifadhi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1999 ikiwa katika milima ya Tenasserim katika jimbo la Prachuap Khiri Khan, inapokea jumla ya watalii 20,000 kwa mwaka huku asilimilia 20 ya watalii ni wa ndani. Alisema ujio wa watalii hao huiingizia nchi yao kiasi cha fedha za nchi hiyo milioni mbili kwa mwaka, ambayo ni sawa na shilingi za Tanzania milioni 150.

Petchkong, alisema hifadhi hiyo imekuwa ikipata umaarufu kutokana na kuwapo kwa mazingira mazuri ya kuishi aina mbalimbali za wanyama, ndege pamoja na mimea mizuri na ndiyo mbuga yenye tembo wengi nchini humo.

“Ulinzi wa wanyapori pamoja na maliasili ndani ya Hifadhi ni madhubuti kwani kuna askari wengi ambao hufanya doria kila mara ndani ya hifadhi na angani kwa kutumia helikopta na wapo katika makundi manne huku kila kundi likiwa na askari wanne hadi sita.”

Katika kuhakikisha zoezi la kumaliza migogoro hiyo linafanyika kikamilifu, mmoja wa wasimamizi wa hifadhi hiyo alisema umewekwa utaratibu wa kuwalipa wanakijiji shilingi 7,500 za Thailand kwa mwezi ili kushiriki katika ulinzi hasa nyakati za usiku.

“Hii ni katika jitihada za kujaribu kutafuta suluhu ya kukabiliana na migororo hii kwani imekuwa ni changamoto na kuna nyakati huwa inakuwa na madhara makubwa kwa uharibifu wa mashamba na makazi pia,” alisisitiza msimamizi huyo Pamoja na mambo mengine hifadhi hiyo ina mkakati wa kuajiri wanakijiji 36 na wakulima kutoka vijiji vya karibu kama vile Yan Sue na Ruam Thai ili kushirikiana kikamilifu na askari wanyamapori katika ulinzi wa hifadhi.

Wanna Kerdsap mwanamama anayeishi katika kijiji cha Ruam anasema kuwa kwa upande wao kama wanakijiji wamekuwa wakiathirika sana na tembo haswa wanapoharibu mashamba yao ya mananasi, lakini wamekuwa wakijtahidi kuwarudisha hifadhini tembo hao kupitia doria zao wenyewe haswa nyakati za usiku.

“Huwa tunajitolea kuwalinda hao tembo na mara tunapowaona huwa tunawafukuza kwa namna ambayo tunahakikisha hatuwajeruhi na wakati huo huo kuhakikisha kuwa hatuwabugudhi kiasi cha wao kukasirika na kutaka kujihami,” Kerdsap anaongeza kuwa kwa sasa wanazishukuru mamlaka husika kwa kuweka kamera kwenye njia za tembo kwani imerahisisha zoezi la kujua wako wapi na wanatokea

upande gani, hiyo ikiwa ni tofautii na zamani ambapo walilazimika kushughulika na tembo pale wanapowaona na pengine wakiwa tayari wamo mashambani mwao na wakiwa wameshaharibu karibu kila kitu.

Jitihada hizo zinazofanywa na Thailand zinashabihiana na zile zinazofanywa na Tanzania, kupitia mashirika ya TAWA, TANAPA na NCAA kwa kushirikaina na halmashuri za wilaya na wadau wengine ambao kwa pamoja wameendelea kufanya doria za kudhibiti wanyamapori kutoingia kwenye makazi ya watu. Tanzania imeweka vituo vya askari katika maeneo yenye changamoto, kutumia teknolojia mbalimbali pamoja na kuweka uzio wa umeme na kuwavalisha mikanda ya kielektroniki (collar) tembo ili kufuatilia mienendo yao na kuwadhibiti wanapotoka ndani ya hifadhi kabla ya uharibifu kutokea.

Aidha Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk. Hamisi Kigwangalla katika moja ya hotuba zake alisema kuwa Wizara itashirikiana na wadau katika kuendelea kutatua migogoro iliyopo katika maeneo ya hifadhi.

TANAPA kwa upande wake imetakiwa kutoa elimu kwa jamii na kuwezesha uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji 95 vinavyopakana na hifadhi za Taifa za Kilimanajro, Arusha, Mkomazi na Saadani.

“Kazi nyingine ni kusafisha mipaka yenye urefu wa kilomita 896 na kuweka alama 25 za kudumu za mipaka kwenye hifadhi za Taifa za Saadani, Burigi, Biharamulo, Kimisi na Ziwa Manyara.

Waziri Kigwangalla aliongeza kuwa, “Mgogoro wa mipaka na vijiji saba vya wilaya ya Serengeti (Hifadhi ya Serengeti) utashughulikiwa na kutoa fidia kwa wananchi wa vijiji 33 vya Usangu (Hifadhi ya Ruaha), Kiliani (Hifadhi yaMahale) na Kimotorok (Hifadhi ya Tarangire).”

Aidha, alisisitiza kuwa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) itaendelea kushirkiana na Tume ya Taifa ya matumizi Bora ya Ardhi (NLUPC) kutayarisha mipango shirikishi ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 100 vinavyozunguka misitu ya hifadhi.

“Ulinzi wa misitu 106 ya Hifadhi utaimarishwa kwa kupima upya na kuhakiki mipaka yenye urefu wa kilomita 759.4, kusafisha kilomita 408.2 na kuweka vigingi 3,825 na mabango 1,016.”

Hitimisho Mikakati ya kupunguza hasara za mazao kutoka kwa tembo inapaswa kutumia busara na sio kuua tembo wala kuwadhuru kwa namna yoyote ile kwa maana haisaidiii kwenye kupunguza hasara ya mazao.

Na kufanikiwa kutokomeza migogoro hiyo inahitajika ushirikiano kati ya wanajamii na wahifadhi ambao wanapswa kujitolea pia ufanisi katika utekelezaji. Mbinu hizi zinatoa matokeo mazuri ya kuboresha fursa za wakulima na tembo kuwa na uwezo wa kuishi bila migogoro.