Home Uchambuzi Natamani kujua vigezo vya vetting za viongozi wetu

Natamani kujua vigezo vya vetting za viongozi wetu

4217
0
SHARE

Hawa kina Charles wanatia huruma sana lakini wengi wanadai hawakuonewa ni haki yao kabisa wame-perform under standards, Tanzania inatakiwa ikimbie hasa kwani tumechelewa katika maendeleo. Swali linaloniumiza kichwa hawa kina Charles na wengineo wamefikaje hapa?

Tunaangalia nini tunapotafuta kiongozi? Ngoja niwakumbushe kwa wachina ambao ni marafiki zetu.

Niliwahi kumsikiliza Zhang Weiwei Mkuu wa chuo kikuu cha Fudah University China. Ni mtu pekee ambaye ameoanisha maendeleo ya China na viongozi wake. Aliwahi kuelezea ni kwa namna gani China inapata viongozi wake.

Weiwei anasema kuwa viongozi wote wa China lazma wapitie mchakato unaojulikana kama selection plus election. Yaani kabla ya kuwa kiongozi china lazma mchakato wa kuwachuja ufanyike kwa kuangalia ulishawahi kufanya nini kabla. Huku kwetu tunasema vetting.

Maeneo muhimu wanayoangalia ni uwezo wako wa kupambana na Umaskini, uwezo wako wa kutengeneza ajira, uwezo wako wa kuyatunza mazingira na uwezo wako katika local economic growth.

Wanawapima toka wakiwa huku chini yaani ngazi za chini anadai viongozi sita kati ya saba ambao ni top kabisa katika serikali yao wamepitia mchakato huo na wamepimwa toka wakiwa katika ngazi za chini za kiuongozi. Na mara nyingine wanakufuatilia toka ukiwa mdogo wanaangalia uwezo wako wa kupambana na mambo ambayo ni vigezo vya vetting yao.

Kila nchi ina vigezo vyake china wao wanaangalia sana swala la ajira, uchumi na mazingira ukifiti haya wabakuchukua. Sijui vigezo vya hapa kwetu vipoje.

Wao wachina wanacriticize mfumo wa Westerns ambao mtu anatokea from nowhere anakuwa kiongozi. Hapa anatoa mfano wa Trump na Bushi kuwa hawakupaswa kuwa viongozi kabisa.

Tanzania hali ipoje? 

Kwa Tanzania kwenye vyama vyetu ambayo ndio kapu la kupata viongozi kuna vijana wa aina tatu.

 

  1. Kundi la kwanza la vijana ni kundi ambalo lipo kwenye chama ili siku wakiwa viongozi watoe huduma. Kundi hili linaamini katika ukweli na sio watu wa kujipendekeza sana kwa ajili ya kupata madaraka. Nyeus huiita nyeusi na nyeupe ni nyeupe. Kundi hili halipendwi sana na viongozi walio madarakani na kama upo katika kundi hili ili uwe kiogozi wa kuchaguliwa au kuteuliwa lazma upambane haswa. Kundi hili hubadilishwa jina na kuitwa wasaliti.

 

  1. Aina ya kundi la pili la vijana ni kundi linalosubiri uteuzi. Hawa hujiunga na chama ili wateuliwe wawe waheshimiwa, chochote utakachomwambia afanye atafanya ilimradi tu ateuliwe. Hawa kuanzia asubuhi hadi jioni, kuanzia january hadi Disemba yeye ni kusifia tu ili aonekane ateuliwe. Hili ndio kundi pia linalotoka wahamiaji na wahamaji. Wote kwa pamoja wanakutana kwenye lengo moja la kupata madaraka. Baada ya kuyapata huwa na mzuka na madaraka na kazi yao kubwa ni kumfurahisha aliyewateua kwa kufanya kazi kwa sifa bila kufuata taratibu za uongozi bora na utawala bora . Huachana na Job Description na kupuyanga kivyao…. Ndio hawa wazee was matamko.

 

  1. Vijana kundi la tatu ni wale waliopo kwenye vyama na wanapata madaraka kwa kuwa tu baba yake au mama yake aliwahi kuwa kiongozi. Hawa ni wale wazee wa mbeleko ukiingia nao kwenye kinyanganyiro utashindwa tu… hawa wana miundombinu mingi ya kuwa viongozi. Hawaamini sana katika ushindani, tuliona hili katika kupitisha majina ya kugombea ubunge Afrika Mashariki. Watu walikuwa wanalia haswa…. sisemi kuwa hawafai kuwa viongozi bali ni vigumu kushindana nao watakushinda tu. Swala la uwezo unakuja kama kigezo cha pili cha kumteua lakini cha kwanza ni mtoto wa nani hii kwao inatosha sana.

Katika makundi yote matatu hapo kundi number mbili na number tatu ndio hukidhi matakwa na hufanikiwa kweli kuwa viongozi.

Lazma tufike mahali tuoanishe umaskini wetu na aina ya Viongozi tulionao. Tanzania yenye rasilimal nyingi namna hii tunashindwaje kutoa huduma za Afya bure kwa watu wetu wote? Tunashindwaje kumaliza tatizo la maji?

Leo kina Charles wanaenda kukutana kule kwa wabunge wenzao. Tufanye vetting badala ya betting. Tutabadilisha mpaka lini? Mnaohusika na vetting mna nafasi kubwa sana ya kumsaidia Rais kupata wasaidizi wanaokidhi matakwa na matarajio yetu kwa muda mrefu. Tunapaswa kukimbia haswa…