Home Makala Kimataifa NGOMA INAPIGWA BRUSSELS, WANACHEZA LUBUMBASHI

NGOMA INAPIGWA BRUSSELS, WANACHEZA LUBUMBASHI

5856
0
SHARE

NA MBWANA ALLYAMTU


Imran Khan, mwana chama wa chama cha PTI ameshinda uchaguzi uliofanyia hivi karibuni nchini Pakistan.  Imran mcheza kriketi huyo maarufu, amevishinda vyama vikubwa nchini vya Muslim League na Pakistani People’s Party.

Japo anaitaji ushirika, ili kuunda serikari ya mseto kwenye taifa hilo lenye umri wa miaka 71 tangu ijitawale mwaka 1947. Pakistan ilitawaliwa na Uingereza.

Wakati hayo yakitokea huko Karachi mji mkubwa wa kibiashara, huku Afrika rais wa nne wa Kongo (DRC), Joseph Kabila Kabange, ametakiwa na mataifa ya Magharibi atangaze kwamba hatagombea tena nafasi ya urais.

Kongo ni taifa lenye utajiri wa  mkubwa wa rasilimali barani Afrika na duniani, limeanza kupata shinikizo kwa sababu wakubwa wanatamani rasilimali zake. Lakini Kabila amekaa kimya.

Ni litu gani kimemfanya Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Konhen kutoa tahadhri kuhusu utawala wa Kinshasa?

Ikumbukwe kuwa mapema mwaka 2014/15 baada ya Joseph Kabila kumtengenezea mazingira ya kumzuia Moise Katumbi Chopwe, kutoshiriki uchaguzi wa DRC, haraka sana mataifa ya Magharibi yalitengeneza kibaraka ambaye wanataka awe mrithi wa Kabila. Mataifa hayo yamemuandaa Jean Pierre Bemba Gombo, ambaye Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (ICC) ya The Hague mchini Uholanzi, imemwachia huru hivi karibuni, baada ya kutumikia kifungo kwa makosa ya jinai ya kivita, aje kumtoa madarakani Joseph Kabila.

Mkakati huu ndio uliotumika mwaka 2011 katika kile kilichoitwa “Operation Arabic Spring” ambayo ilizikumba nchi za Afrika Kaskazini. Nchi za Magharibi zilimuandaa Mohammed Ali Baradei,  kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak, ingawaje mkakati wao uligonga mwamba kwani chama chenye mrengo mkali—Muslim Brotherhood kushika hatamu mwaka 2012 likishinda katika uchaguzi mkuu—jambo  ambalo nchi za Magharibi hazikuridhika nalo. Zikatekeleza mapinduzi haramu ya tarehe 13/7/2013na kuondosha utawala wa kiraia wa Rais Mohamed Morsi kupitia maandamano ya  “Operesheni Taharir Square ya Pili”, baada ya kwanza kushindwa.

Mkakati huu unaofanywa huko DRC na mataifa ya kibepari, ambayo yanamtaka Jean Pierre Bemba Gombo awe kibaraka wao kwa kutekeleza mikakati “Mujarabu” ya kuitafuna Kongo na kunyonya madini yake. Ama kweli akutafutae hachoki kabisa. Hivi ukweli hawakuridhika walipotekeleza Operation Barracuda iliyo ondosha uhai wa Baba wa Taifa, Patrice Lumumba mwaka 1960 pamoja na mauaji ya mwaka 2001 yaliyosababisha kifo cha Laurent Desire Kabila, rais mzalendo, aliyeamua kusaliti makubaliano ya mabeberu kwa kutupilia mbali “mkataba wa Lemela” bila kujali hatari yake naye aliuwawa kwa kipigwa risasi na vijana wake kupitia kile kilichoitwa “operation Nyamrenge”.

Huyu Jean Pierre Bemba Gombo, ametangaza kuwa atawania urais katika uchaguzi mkuu ujao. Bemba alikuwa ni kiongozi wa kundi la waasi lilojulikana kama MLC. Kundi hilo liliongoza maasi mashariki mwa Kongo katika majimbo ya Kivu ya Kaskazini, Kivu ya Kusini, pamoja na Jimbo la Mashaliki. Pia huyu Bemba aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa Kongo.

Kuachiwa huru kwake kutoka kifungoni Ulaya, na kufutiwa mashitaka yote  na ICC kuna ashiria nini? Ni nani huyu Bemba? Kupitia makala haya, inaonesha kwamba Ulaya na Marekani kamwe hazijawahi kulala.

Huyu Bemba anayeonekana kung’ara katika mbiu hizi za urais huko Kongo, anatoka katika kabila la Ngala (kabila alilotoka pia rais muda mrefu, Mobutu Seseseko). Jimbo hilo lipo Mashaliki ya Kongo na lina makabila manne (4) makubwa ya Kongo.

Bemba alikamatwa na maofisa usalama huko  Brussels, Ubeligiji Mei 24, mwaka 2008, ambako ndiko kichaka na kimbilio kuu ya vibaka, vibaraka, wahalifu na maharamia wengi wa Afrika.

Hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Bemba ilitolewa na ICC na Juni 3, mwaka 2008, na akajisalimisha Juni 15, mwaka 2009. Majaji wa ICC walithibitisha mashtaka dhidi yake, kisha kesi ilianza kusikilizwa November 22, mwaka 2010, na kesi kufungwa November 12 na 13, mwaka 2014.

Awali waendesha mashataka wa Mahakama hiyo, waliiomba imuhukumu kifungo cha miaka isiyopungua 30 jela, kutokana na makosa aliyokutwa nayo. Licha ya upande wa utetezi kudai kuwa mteja wao hakuhusika kwa vyovyote vile kutekeleza uhalifu dhidi ya binadamu, majaji walijiridhisha pasipo na shaka, kuwa Bemba alishiriki kwenye kuamrisha askari wake kutekeleza uhalifu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Kongo na Afrika ya Kati wakimtetea kwamba katika mashitaka hayo Bemba hakuwa peke yake na kwamba hukumu hiyo inaweza isiwe tiba ya wahanga wa vitendo vya ubakaji na udhalilishaji, ingawa ndani ya Mahakama, Bemba mwenyewe alikiri na kuomba radhi na kutaka apunguziwe adhabu.

Bemba alishitakiwa kwa makosa ya Oktoba 2002, na Machi 2003, kwa kumuunga mkono Rais Ange-Felix Patasse aliyekuwa akikabiliwa na jaribio la kupinduliwa na Jenerali Francois Bozize, ambaye baadaye alikuja kuwa Rais wa Afrika ya Kati.

Kuachiwa kwa Bemba wakati huu, ni mkakati na Mpango Maalumu wa Ulaya na Marekani, ili aje agombee urais  katika uchaguzi ujao nchini Kongo. Kupitia mkakati huu, nimejaribu kuutazama kwa makini, na kujikuta nikijisemea mwenyewe maneno: “Kutokana na uroho wa mataifa ya Magharibi juu ya Kongo, kamwe hakuna kiongozi mzalendo atafanikiwa kuiongoza Ikulu ya Kinshasa (Palace de national), na siku Kongo ikatulia, basi ujue kuwa Dhahabu na madini yote yatakuwa yamemekwisha na kubaki kahandaki ya kujizikia kizazi kijacho cha Kongo.”

Maana alipo jitokeza mzalendo Lumumba walimwua. Akaja kibaraka Mobutu akatafuna nchi kwa kugawana na hao mabeberu. Walipomchoka, wakamtema kama ganda la mua lililokwisha utamu. Wakamfadhili Laurent Kabila kupitia vuguvugu la Wanyamlenge waliokuwa wakidai haki zao huko Mashaliki mwa Kongo. Naye alipofanikisha kuingia Ikulu ya Kinshasa, akawageuka mabeberu, akaamua kuwatumikia wananchi wa Kongo, naye akauwawa.

Akaletwa Joseph Kabila Kabange, mtoto wa Andrea Christopher Kanambe, aliye lelewa na Mzee Kabila. Huyu Joseph Kabila Kabange ambaye ni Mnyarwanda kiasili, akashika nchi kama kibaraka wa mabeberu,  na yeye sasa wameanza kumchoka.

“Ngoma inapigwa Brussels, Washington, London na Paris, viuno vinakatwa Lubumbashi (eneo ambalo ndio chimbuko la ngoma za Rumba). ” GOD have Mercy upon us, remove this shame from us—Mungu tusaidie, utindolee hii asibu.

Ama kweli maneno ya muasisi wa taifa la Kongo, Waziri Mkuu wa kwanza, Patrice Emiel Lumumba, jemadari wa haki wa Afrika, alivyosema mwaka 1960:

“Uhuru wa kisiasa katika nchi hauna maana yoyote, iwapo hakuna Uhuru wa kiuchumi na maendeleo ya kijamii”

Udhibiti uliofanywa na Joseph Kabila dhidi ya Moise Kitumbi, ni mkakati wa kumzuia katika harakati zake za kisiasa. Katumbi anatajwa kuwa kipenzi cha watu wengi huko Kongo, kutokana na juhudi zake za kizalendo alizozifanya alipokuwa Gavana katika jimbo la Katanga.

Katumbi ambaye ni Mkongomani mwenye uchotara wa Ureno, anatoka katika kabila la Luba linalo patikana na Katanga, ambalo zamani liliitwa Shaba. Jimbo hilo linatajwa kuwa ni tajiri zaidi huko Kongo.

Je unajua ni kwanini ameandaliwa Jean Pierre Bemba? Na je, kwa nini Moise Katumbi Chipwe hahitajiki? Je, unajua mkakati unaosukwa huko Kongo na mataifa ya Marekani, Uingereza, Ufaransa?.  Na mkakati huu utafanikiwa? Na je, Joseph Kabila atasalia madarakani?.

 

Endelea kunifatilia katia gazeti huli la RAI.

+255679555526.Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com