Home Makala Kimataifa Obote, Museveni wamepindua Katiba

Obote, Museveni wamepindua Katiba

2766
0
SHARE

KAMPALA, UGANDA

ZIMWI la mapinduzi lililowahi kuliandamana bara la afrika katika kipindi cha miaka 50 iliyopita kwa sasa limepungua. Hakuna mapinduzi ya jeshi katika nchi za kiafrika, lakini ipo dhana nyingine ya kupindua nchi bila umwagaji damu.

Miongoni mwa waliowahi kufanya mapinduzi dhidi ya Katiba ni aliyekuwa Rais wa Uganda, Milton Obote. Obote ni miongoni mwa wanasiasa waliochukua jukumu ya kuitupilia mbali Katiba ya wananchi na kujimilikisha utawala wan chi pasipo matakwa ya wapigakura. Kwmaba hapakuhitajika uchaguzi ili kumpa mamlaka ya kutawala kama ambavyo demokrasia inavyotaka.

Tukio la kupinduliwa katiba lilifanyika miaka 50 iliyopita na Milton Obote ambaye wananchi wa Uganda walifanya sherehe za kumbukumbu kumkumbuka rais huyo wa zamani. Milton Obote aliisimamisha katiba na kujigeuza mtu muhimu zaidi nchini Uganda, uamuzi ambao uliibadili mweleko wa historia ya Uganda na kushawishi mustakabali wa taifa hilo mpaka leo hii.

Rais Yoweri Museveni au Iddi Amin kabla yake, historia ya Uganda imeghubikwa na watu walioingia madarakani kwa msaada wa kijeshi, hali ambayo inachangia kuwa na mfumo tofauti wa kidmokrasia ambao unamlazimisha rais kutoachia madaraka upesi au kuruhusu demokrasia kongwe kutawala ndani ya mataifa yao.

Si Museveni peke yake hata jirani yake Rwanda, Paul Kagame ametumia mbinu ya kupindua Katiba hali ambayo imesababisha wananchi waone hakuna kiongozi mwingine thabiti kuliko Kagame na Museveni.

Nchini Uganda mwanasias wa kambi ya upinzani kama Kizza Besigye amekuwa katika mapambano ya muda mrefu kuhakikisha taifa lao linakuwa kwenywe mkondo wa demokrasia iliyokomaa au kuachiwa ichukue nafasi yake.

Aidha, Uganda haijawahi kubadilishana madaraka kwa njia ya amani, kwani tangu 1986 imekuwa ikitawaliwa na Yoweri Museveni hivyo kila uchaguzi anaibuka mshindi.

Msingi wa jambo hilo uliwekwa na Milton Obote. Aprili 15, 1966 sawa na miaka 50 iliyopita, Obote aliisimamisha katiba ya Uganda na kujitangaza kuwa rais. Tukio hilo lilimaanisha Obote alifanya mapinduzi dhidi ya Katiba ya nchi hiyo.

Aidha, alimlazimisha kwenda uhamishoni Mfalme wa Baganda Edward Mutesa II, na rais wa Uganda wakati huo. Kabila la Baganda lililopendelewa zaidi na Wakoloni wa Kiingereza.

Akiwa Naibu waziri mkuu wa Uingereza wakati wa Ukoloni, Winston Churchill  alisema kabila la Baganda walikuwa watu wastaarabu. Ni ufahamu huu kwamba Baganda walikuwa watu maalumu, uliochochea harakati za Wasomi wa Kiganda kutaka madaraka.

Milton Obote alikuwa mtu wa Kabila la Walang’o kutoka kaskazini mwa Uganda, na alikuwa akipinga madai ya Baganda kuwa na haki za kuchukuwa madaraka na pia urithi wa zama za ukoloni.

Kupitia muungano wake wa Uganda People’s Congress (UPC) uliokuwa na wanachama kutoka nchini kote, lifanikiwa kushinda wingi bungeni. Tofauti na Kabaka Mutesa aliyekuwa na maono ya kuendeleza utamaduni wa ukoloni, wanasiasa wa wakati huo waliona fursa kwa Obote kuweka mwanzo mpya.

Fikra zake za kisiasa alizipata nchini Kenya, ambako alikuwa bega kwa bega na rais wa baadaye wa taifa hilo mzee Jomo Kenyatta kuongoza mwamko mpya wa Kiafrika.

Kwa kumpeleka uhamishoni mfalme wa Buganda, Obote alijihakikishia uungwaji mkono wa raia wa Uganda kutoka eneo la kaskazini na pia waliokuwa katika maeneo mengine ya Uganda wasio na uhusiano na ufalme wa Buganda.

Historia inasema mapinduzi ambayo yalisababisha kukosekana serikali za kiraia. Hata hivyo mwaka 1971 Obote alipinduliwa na Iddi Amin na akakimbilia uhamishoni nchini Tanzania, ambako alianza harakati za kutaka kurudi madarakani tangu mwaka 1980, kabla ya kuondolewa tena miaka sita baadae na rais wa sasa Yoweri Museveni.

Museveni mwenyewe ambaye alitokea kwenye tawi la vijana la chama cha Obote cha UPC, ametumia njia mbalimbali kuzigawa jamii ambazo Obote alizihodhi kabla yake.

Kupitia jeshi lake la waasi ambao kwa sehemu kubwa walikuwa wanatokea Magharibi mwa Uganda, alifanikiwa kulishinda jeshi la serikali lililokuwa linadhibitiwa kwa sehemu kubwa na maafisa kutoka kaskazini hasa Walango na Wacholi.

Kuanzia mwaka 1986 Museveni alifanikiwa kujenga mfumo ambao unamhakikishia kukaa madarakani mwa miongo kadhaa. Lakini mbinu zake zinafanana sana na za Obote kwa njia kadhaa.

Katika mapambano dhidi ya kundi la waasi wa LRA kaskazini mwa Uganda, Museveni anarudia ulinganifu kati ya makundi ya wakaazi mbalimbali, na anaongeza bajeti ya jeshi kila mara.

Na kama ilivyokuwa kwa Obote, anawaacha huru wanajeshi wake, hata wakati baadhi yao wametuhumiwa kwa kufanya unyama kaskazini mwa nchi.