Home Habari Profesa Lipumba amgeuka Magufuli

Profesa Lipumba amgeuka Magufuli

2536
0
SHARE

lipumba na magufuliGABRIEL MUSHI, SHABANI MATUTU

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Prof Ibrahim Lipumba, amemgeuka Rais John Magufuli kwa kusema Serikali yake inatesa watu na imekurupuka kufanya uamuzi wa kuwabolea Watanzania wasio na hatia.

Profesa Lipumba, ni miongoni mwa wanasiasa wachache wa upinzani waliotoa kauli za kumpongeza Rais Magufuli siku chache mara baada ya kulihutubia Bunge.

Mchumi huyo alipata nafasi ya kumtembelea Rais Magufuli Ikulu, Novemba 30, mwaka jana, ambapo katika mazungumzo yao, mbali ya kumpongeza kwa kuchaguliwa, lakini pia alimsifia kwa kutoa hotuba nzuri iliyoweka mwelekeo mpya wa Serikali ya awamu ya tano bungeni.

Katika ziara hiyo Prof Lipumba alisifu na kuunga mkono juhudi za Rais katika kupambana na wakwepa kodi na wahujumu uchumi.

Hata hivyo juzi, Profesa Lipumba alibadilika na kuikosoa Serikali ya Magufuli kutokana na kitendo chake cha kuvunja nyumba za wananchi wake.

Akizungumzia na RAI kwa njia ya simu, Profesa Lipumba alisema Serikali ya Rais Magufuli imekurupuka kuchukua hatua hizo na kwamba sheria haiwezi kuchukuliwa kwa kushurutishwa namna hiyo.

Alisema si jambo baya kutekeleza matakwa ya sheria, lakini katika utekelezaji wa suala hilo ni lazima kuwa na ubinadamu.

“Lazima tutambue kuwa watu wengi wanaoishi katika nyumbani hizi za mabondeni ni wapangaji, si wenye nyumba, hawa wamekwenda kupanga katika maeneo yale  kwa sababu kulikuwa na huduma zote muhimu za kijamii kama vile maji na umeme.

“…pili kuna watoto ambao hawakuchagua wazazi wa kuwazaa,na ni lazima uzingatie haki za watoto. Utakapohamisha watu lazima uwajengee mazingira ya kuishi, kwa sababu watoto hawana makosa,”alisema.

Alisema amesikitishwa na ukosefu wa ubinadamu unaofanywa na Serikali ya Magufuli, na kwamba hali hiyo inaweza kumkwamisha katika mbio zake za kisiasa na ndio maana hata CUF walipinga operesheni hiyo kupitia mbunge wao wa Kinondoni.

Alisema wakati Rais akisimamia kauli yake ya Hapa Kazi tu, wao wanasimamia kauli ya Hapa haki tu.

AKOSOA UTEUZA MAKATIBU WAKUU

Katika hatua nyingine Profesa Lipumba alielezea kushtushwa na kustaajabishwa na wingi wa makatibu wakuu walioteuliwa Rais Magufuli.

Profesa Lipumba, aliusema hana shida na Rais Magufuli kwenye uamuzi wake wa kuunganisha wizara kwani jambo hilo liliwahi kufanyika katika Serikali ya awamu ya kwanza iliyokuwa chini ya Hayati, Mwalimu Julisu Nyerere.

“Suala la kuunganisha wizara si jambo baya kwani hata miaka ya 1960 na 1980 wizara ya Kilimo ilikuwa pamoja na Mifugo na uvuvi, sawa na hii ya Mawasiliano, Uchukuzi na Ujenzi, lakini kitendo cha kuweka Makatibu Wakuu wawili mpaka watatu katika wizara sita zilizounganishwa kimeonesha namna gani Rais Magufuli amekosea katika hili,”alisema.

Alisema hakuna kitu cha namna hiyo katika uongozi, ni jambo la ajabu kwa waziri mmoja kuwasimamia makatibu wakuu watatu.

“Tunapaswa kufahamu kuwa msimamizi mkuu wa Wizara ni Katibu Mkuu sasa wakiwemo makatibu wakuu watatu hapo lazima kuwepo na mvurugano wa kiutawala kwa sababu katika wizara Katibu Mkuu ndiye mhimili, waziri ni kiongozi wa kisiasa tu,”alisema.

“Sijui nani aliyemshauri kufanya hivi, kwa sababu hali hiyo inasababisha kutokea kwa mvurugano ambao watu wataanza kutafsiri kuwa kasi yake aliyoanza nayo ni nguvu ya soda.”

Alisema kitendo cha Katibu Mkuu mmoja kuwa na Manaibu watatu si tatizo katika hilo, lakini ukiwapa makatibu wakuu watatu kila mmoja idara yake lazima gharama ziongezeke kwa maana ya mishahara, bajeti za idara yake kama ni makamishna wa kilimo, mifugo au uvuvi.

“Ni wazi huwezi kuwa na uongozi wa aina hii kwani utaleta vurugu,”alisisitiza.

TAARIFA ZA KUMSHAURI RAIS

Pamoja na mambo mengine, Profesa Lipumba alikana madai ya kuwa miongoni mwa washauri wa Rais Magufuli kwenye masuala ya uchumi.

“Nilioni watu wanaandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa Rais Magufuli ameniteua kuwa mshauri wake wa masuala ya kiuchumi, si kweli hata kidogo, hilo halikuwa ajenda yetu pindi nilipokwenda kuonana naye Ikulu.

“Kiujumla Magufuli ni mtu mwepesi kuelewa jambo, anasikiliza, ni mtu ambaye pia anashaurika,  lakini hatukuzungumzia kabisa suala la mimi kuwa mshauri wake wa masuala ya uchumi,”alisema.

BOMOA BOMOA YAIBUA MAPYA

Wakati zoezi la bomoa bomoa likisitishwa, kumeanza kuibuka madai ya baadhi ya nyumba kubolewa kimakosa.

Makosa ya namna hiyo yanatajwa kufanyika katika majengo ya Mwenge kijijini mkabala na maghorofa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Akizungumza kwa masikitiko kuhusu namna walivyobomolewa nyumba hizo kimakosa kwa niaba ya wenzake tisa, Clemence Mashamba alisema nyumba hizo zimebomolewa kwa kukiuka sheria.

Akizungumzia kuhusu eneo hilo alisema nyumba zao zilikuapo kisheria zikwia na hati moja ya kijiji ya mwaka 1989 iliyokuwa chini ya Chama Cha Ushirika Cha Ujenzi wa nyumba, Mwenge.

“Kwa mfano nyumba yangu kama unavyoona nyaraka inaonyesha ilikuwa ni kiwanja C1, na nilikuwa nalipia kodi tangu nilipopewa mwaka 1989,” alisema Mashamba.

Mashamba alisema eneo hilo walikaa kwa hati hiyo ya kijiji kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 2002 alipojitokeza tajiri mmoja aliyeonyesha nia ya kutaka kulinunua na wao kumkatalia na kuamua kulifuatilia Manispaa.