Home Latest News RAWLINGS: Nguzo iliyoisimamia Ghana kisiasa, kiuchumi

RAWLINGS: Nguzo iliyoisimamia Ghana kisiasa, kiuchumi

2560
0
SHARE

NA ALOYCE NDELEIO

KATIKA kipindi cha miaka 20 tangu alipoachia madaraka hakuna jambo ambalo limejitokeza au kuingilia katika kutaka kuwagawa Waghana na hali hiyo imetokana na misingi mizuri aliyowaweka wananchi wa Ghana na anaonekana kuwa ni mtu wa pili baada ya muasisi wa taifa hilo, Kwame Nkurumah.

Huyo si mwingine bali ni Flt. Lt. Jerry John Rawlings ambaye Novemba 12, 2020 alifariki dunia.

Kauli hiyo inasadifu kumlenga yeye kutokana na mtiririko wa historia kwamba kati ya mataifa yaliyokumbwa na mapinduzi ya kijeshi barani Afrika na hususani Afrika Magharibi Ghana na Nigeria yalikuwa ni mambo yasiyoepukika.

Hata hivyo katika mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na Rawlings yalihitimishwa kuwa ni mwanzo wa safari ya kurudi katika Kanani aliyokuwa ameianzisha Rais wa Kwanza wa nchi hiyo, Kwame Nkurumah.

Inakuwa rahisi kusema hiyo kutokana na utendaji wa Rawlings ambao ulionesha dhahiri kuwa lengo lake lilikuwa ni kuleta mabadiliko ya kijamii kisiasa na kiuchumi kwa wananchi wa Ghana baada ya kukumbwa na mapinduzi ya kijeshi ambayo  yalikuwa yanazidi kuwanyongesha wananchi.

Miaka mitatu iliyopita Mwandishi wa makala hii alibahatika kukutana na Mwandishi Samuel Duodu kutoka Ghana katika safari iliyowakutanisha Makao Makuu ya Shirika la Chakula Duniani (FAO) Roma, Italia na katika mazungumzo baina yao aliweza kupata uhalisia wa hali ya Ghana kutoka kwa raia wake.

Kimsingi ni kwamba pamoja na Mwana wa Afrika Kwame Nkrumah, alimweleza Duodu anavyovutiwa na Rais Mstaafu Jerry Rawlings  ambapo alibainisha kuwa kiongozi huyo ndiye aliyeipa Ghana sura mpya iliyonayo leo hii.

Pamoja na mambo mengine kuhusu tamaduni ambazo sehemu kubwa  zilionesha kufanana na Tanzania ukweli uliojionesha wazi kuwa kama sio uongozi wa Rawlings mambo yangeweza kwenda mrama.

Ikilinganishwa na tawala nyingine za kijeshi zilizotokea nchini humo wengi wakiwemo wanataaluma wamekuwa wakisema kuwa  hawajui ni kwa namna gani wamtambulishe au wamchukulie Rawlings.

Wengine wamekuwa wakijiuliza iwapo ndiye shujaa aliyeaminiwa kuwa na uzalendo na Ghana au ni mtu aliyetumwa kuharibu muundo wa utawala uliofuata baada ya ukoloni?

Hata hivyo Rawling alikuwa ni nguzo ya msingi na mhimili wa bahati ya Ghana kisiasa na kiuchumi.

Ghana ilihama kutoka utawala wa kijeshi hadi kuingia katika  mfumo wa utawala kidemokrasia  ndani ya chaguzi mbili za mwaka 1992 na 1996 na zote zikiwa na matokeo ya ushindi kwa kiongozi wa zamani wa kijeshi Flt Lt Jerry Rawlings akiwa kama Rais.

Chama cha Rawaling kilipata viti vingi vya Bunge katika chaguzi zote mbili. Lakini hilo halikuwa ni jambo rahisi kutokana na dhana kwamba ni utawala wa kiimla ulikuwa unajaribu kujihalalisha wenyewe  kupitia uchaguzi kama ambavyo imekuwa katika tawala nyingi ndani ya Afrika.

Tofauti na dhana hiyo  kuchaguliwa kwa Rawlings kuwa Rais  kulionesha kwamba inaikubali demokrasia ya kiliberali ambayo ilikuwa na sauti na kuathiri upande wa upinzani kwa kiwango kikubwa ndani ya siasa za Ghana katika miaka ya 1990.

Kwa mara ya kwanza  ndani ya kipindi cha miaka 20, utawala uliokuwa chini ya uongozi  Rawlings uliweza kujibu umma  kwa programu na sera na hali kadhalika taasisi kadhaa za taifa ziliiimarishwa na hata kuwa huru zaidi.

Hata hivyo uwezekano wa kutokea mapinduzi mengine ya kijeshi lilikuwa ni jambo lisiloepukika hususani kama utawala wa Rawlings ungetaka kugombea tena mwaka 2000.

Kipindi hicho ni ambacho kikatiba asingeweza kugombea tena kwa mara nyingine tena, lakini ilikuwa ni vigumu kuwazia kama Ghana ingerudi tena katika hali hiyo.

Badala yake  yalikuwepo mawazo ya kutaka kuongeza muda jambo ambalo kwa serikali na taifa kwa ujumla yalionesha tabia tofauti kwa demokrasia na utawala wa kiimla. Hata hivyo hali ikawa tofauti  nkwa Ghana kuwa moja ya nchi chache zilizonesha kuegemea katika  demokrasia.

Baada ya uhuru wa Ghana mwaka 1957 nilifuatiwa na  muongo wa awali wa kidemokrasia, na baadaye kidikteta chini ya Kwame Nkrumah chini ya serikali ya Chama cha Convention People (CPP) ambayo iliishia mwaka 1966 kutokana na mapinduzi ya kijeshi.

 Baada ya kukabidhi madaraka  kwa serikali ya kiraia iliyochaguliwa jeshi liliibuka tena mwaka 1972. Hayo yalifuatiwa na mapinduzi ya kijeshi chini ya maofisa wadogo mwanzoni mwa mwaka 1979 ambayo yalimwingiza Ft. Lt. Jerry Rawlings madarakani kwa mara kwa kwanza. Hata hivyo  serikali ya kuchaguliwa ya kiraia  ilichukua hatamu baada ya uchaguzi uliofanyika baadaye mwaka huo.

Baada ya miaka miwili ya utawala usio na mafanikio Rawlings alirudi tena madarakani  kupitia mapinduzi ya kijeshi  mwishoni mwa mwaka 1981. Awalia alitupilia mbali ‘mfumo wa kimagharibi’ wa vyama vingi kidemokrasia kwamba ‘haukufaa katika hali ya uhalisia wa Waghana’.

Hata hivyo ndani ya kipindi alichokuwa akishikilia msimamo huo alibadilika na kukubali mfumo wa kidemokrasia. Akiwa amewashinda wapinzani wake kwa kura katika chaguzi za kidemokkrasia mwaka 1992  na kwa mara nyingine tena mwaka 1996, chama chake cha National Democratic Congress kilipata wabunge wengi katika chaguzi zote mbili.

Awamu ya pili ya historia ya Ghana baada ya ukoloni  kutoka mwaka 1981 ni kipindi kinachohusisha uimara kisiasa na kukua kwa uchumi. Hali hiyo imekuwa inaonekana  hata hivi leo kwamba hakuna mtu mwingine aliyeiwezesha zaidi ya Rawlings mwenyewe.

Rawlings awali akionekana kuwa mtu wa vurugu, baadaye utawala wa kiimla  na mwishoni kidemokrasia alitawala kutoka kwenye kutoeleweka hadi kufikia katika uwiano wa kisiasa na uchumi shindanishi uliona uwiano miaka ya 1990 na karne ya 21.

Hali ngumu ya ghasia ilikuwa kwenye awamu ya kwanza ilidumu kutoka mwaka 1982 hadi 1983/84 ambapo msururu wa mikakati ya kisiasa na  kiuchumi ilifanyiwa majaribio bila mafanikio makubwa.

Kuanzia mwaka 1983-84 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990 serikali ilijitahidi kusimamia  uchumi na kuchochea hamasa  ya mabadiliko ya kisiasa  kupitia njia kadhaa.

Ukweli unabakia kuwa serikali ilikuwa ni kali  na haikuwa tayari kusikiliza mapendekezo mbadala  katika kushughulikia matatizo ya nchi.

Hadi mwaka 1992 wakati nchi ilipokuwa ya kidemokrasia sera za uchumi na siasa za Rawlings zilibakia kufunukiwa na  mtindo wa kiimla pamoja na nguvu nyuingi za ukali.

Maamuzi yalifanywa na wachache bila kugatua madaraka akiwemo Rawlings na hali hiyo ilionekana kuwa kundi la wachache  limezichukua taasisi za serikali.

Katika miaka 1980 majaribio ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rawlings yalifanyika kama kawaida. Lakini msingi wa utawala wake kuendelea kuwepo ilikuwa ni udhibiti wa kina wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyokuwa vinamuunga mkono.

Kazi ya vikundi hivyo iliundwa kwa kuhamasisha watu katika kulinda kile ambacho Rawlings alikiita ‘mapinduzi’. Hata hivyo mara nyingine vilikuwa ni mashine za kukandamiza na kuwaponda waliokuwa wanapinga.

Mbinu kali za wanajeshi na watu wa usalama ziliweza kuweka makubaliano na kundi ambazo awali zilikuwa na sauti ya upinzani kisiasa kiasi kwamba utamaduni wa ‘kuwa kimya’ ulikuwepo.

Pamoja na hali hiyo utamaduni huo uliisha. Waghana wengi watakuwa na shauku ya kuona Rawlings anarudi tena. Baadhi watamkumbuka kama kiongozi aliyeona mbali na ambaye aliipitisha Ghana katika viraka vigumu na baadaye kuifikisha nchi katika hali nzuri kuliko ingebakia bila utawala wake.

Hata hivyo kubwa zaidi ni kwamba Rawlings anabakia katika historia ya Ghana kwa kuirudisha katika mkondo ambao uliasisiwa na Mwana wa Afrika Kwame Nkrumah.