Home KIMATAIFA Siasa ni uhai si uadui

Siasa ni uhai si uadui

1185
0
SHARE

ALEX CHIGAITAN -CUBA

KATIKA karne nyingi sasa tumaini kubwa la mwananchi limekuwa siasa. Kama ilivyo mwanadamu katika karne nyingi, amekuwa na tumaini ustaarabu wa binadamu ni kuamini juu ya ustaarabu wa imani ya dini yake. Uhai wa binadamu umebebwa kwa asilimia 76.3 na siasa.

Tunakula kwa sababu ya siasa, tunasafiri kwa sababu ya siasa, tunatibiwa kwa sababu ya siasa, tunalala kwa sababu ya siasa, tunakunywa kwa sababu ya siasa. 

Siasa inapita kwenye moyo wa kila mwananchi. Kama ilivyo imani ya dini kwa mwanadamu. Siasa ni uhai maana inabeba kila kitu kinachomzunguka mwananchi. Hakuna mtu katika dunia hii ya kikomunist na kibepari ambaye anaweza kusema anaishi bila siasa. 

Siasa inatawala dunia, inatawala serikali, inatawala familia, inatawala vijiji, inatawala kila mwananchi tajiri au masikini. Njia pekee ya kiongozi yeyote anayeongoza siasa ni sawa na siasa inayomwongoza mwananchi.

Siasa za leo zimejaa sumu. Sumu zenye afya mbaya kwa uhai wa mwananchi, mwanasiasa yeyote ndani ya moyo wake anapofanya “suistanable politics” anakuwa na haki kwa uhai wa siasa.

Wanasiasa wenzangu kote Afrika. Hasa nchi yangu ya asili Tanzania, tunapaswa kurudia upya dhamira zetu juu ya siasa na kujiuliza ni kweli tumekubali kufanya siasa zenye afya ya sumu na kuacha siasa zenye msingi wa uhai wa watu.

Masikini hasa vijijini, unawezaje kudiriki kufanya siasa, kutafuta cheo au kujulikana wakati kijiji/mtaa wako una umasikini mkubwa. Hakuna Maktaba ya vitabu, hakuna maji, hakuna elimu bora, kuna umasikini uliokithiri, watu  hawana  makazi bora.

Takwimu zinasema katika wanasiasa kumi, nane wamebeba sumu ya siasa. Ni wanasiasa wawili tu wamebaba uhai wa siasa kama afya ya siasa. Kwanini sumu ya siasa? Maana yake Ndani yake kuna siasa za unafiki, siasa za maovu, siasa za uongo, siasa za matumaini hewa, siasa maisha magumu ya wananchi, siasa machafuko ya vita na siasa za kukosoa serikali. Bila ushahidi wa kutosha. 

Hakuna mwanasiasa yeyote mwenye furaha. Kama ilivyo hakuna mwananchi mwenye furaha. Jamii zetu zimekuwa hazina furaha kwa sababu ya siasa zenye sumu. Siasa zenye sumu imekuwa tabia ya binadamu kama daraja la kupanda kufikia mamlaka ya uongozi. 

Vijana wengi Afrika na nchi zinazoendelea. Wamekuwa wanaamini kuwa njia pekee ya kuwa na maisha bora ni kushiriki siasa zenye sumu. Viongozi hawa wakipata madaraka kwa mfumo wa siasa hizi “no turn around on social development”  Hii ni dalili ya mtu anafanya siasa zenye sumu ni nadra sana Afrika kupata viongozi mfano wa Mwalimu Julius Nyerere, mfano wa Rais John Magufuli, mfano wa Jakaya Kikwete, mfano wa Benjamin Mkapa ambao ndani ya nafsi zao wamechagua kufanya siasa za maisha ya watu. 

Wamechagua kuondoa sumu ya siasa ndani ya miili yao na kufanya siasa zenye uhai wa watu yaani maendeleo ya watu. 

Mabadiliko ya fikra kwa wanasiasa vijana leo, wanapaswa kubadilika na kutoka kwenye “unafiki” dharau na kujipendekeza kwenye kundi la siasa zenye sumu na wanapaswa kuchagua kuamini nidhamu na upendo wa siasa ni uhai. Kila mwanasiasa kijana atafanya hivyo hakuna umasikini tutaona vijijini. Kila mtu atawajibika vijijini na kuondoa umasikini.

Umasikini wa macho kwa mwanasiasa mwenye sumu, hawezi kuona, kuhisi wala kugusa. Atashiriki siasa za kudanganya kwa kutoa ripoti mbaya kwa mamlaka za juu kuwa anatekeleza. Kumbe “uongo” kumbe sumu ya kuzalisha umasikini. 

Mwananchi anapitia wakati mgumu sana. Kwa Afrika kuwa na siasa za sumu. Siasa zinazorudisha nyuma maendeleo ya watu. Uhai wa watu Afrika unapotea, watu wanaishi chini ya dola moja ya Marekani jambo ambalo ni mbaya kwa maendeleo ya watu.

Haiwezekani unakuwa na mwanasiasa anaingia kwenye utendaji. Kutafuta majibu ya maendeleo, anawaza kujilimbikizia mali, kuongeza mishahara na posho, watu vijijini hawana maktaba za vitabu, hakuna  (sustainable production). 

Afrika inahitaji kupiga hatua ya siasa ni uhai, tuone maendeleo vijijini, tuone maendeleo ya jamii zetu, tuone msukumo wa matarajio ya uongozi, tuone matarajio ya siasa zetu, tuone majira ya siasa zenye uhai.

Progamu za wanasiasa kwa wastani wa asilimia 62.3 zimekuwa hazina ukweli, zimekuwa zinaandaliwa kuweka umakini hewa na kuwekeza matumaini hewa.

Hii ni changamoto kwa siasa zenye kuleta uhai wa jamii zetu. Ikitokea wanasiasa wameandaa programu za siasa angalau kwa asilimia 3.2 zenye uhai wa siasa zinakuwa na mchango mkubwa kwa taifa.

Nichukulie mfano kwa nchi yangu programu za kisiasa zenye matokeo bora katika hisitoria ya Tanzania. Programu ya “Tanzania ya Kijani” programu hii ni alama kwa taifa imezalisha matokeo bora kwa mwamko wa siasa Tanzania na kuleta uhai wa CCM kuliko wakati wowote.  Matokeo yake imesaidia kuleta taswira ya jamii ambayo inaweza kufanya kazi na kuzalisha.

Vijana wamekuwa na uwezo wa kushiriki siasa za maendeleo. Mfano mwingine wa programu ya siasa ni “siasa ni kilimo” hii ni programu ambayo ilileta mapinduzi makubwa ya mwelekeo wa siasa na mipango ya serikali katika kujitegemea. Kwa taifa hizi ni asilimia chache za siasa za uhai wa watu.

Moja ya programu za siasa zenye sumu kwa Tanzania “operation sangara” hizi ni siasa zilikuwa zinajaribu kujenga jamii mbaya ambayo haijawahi kutokea Tanzania. Matumaini yake yalikuwa ovu watu walipokea uongo, kudanganya aina ya demokrasia kwa taifa, kuzalisha viongozi wanatukana serikali, kuidharau mamlaka ya serikali, kujenga sumu ya siasa, hivyo sote tunaweza kujua jinsi gani? Kuna umuhimu wa siasa zenye uhai kwa jamii zetu. Kuharakisha maendeleo.

Kulinda uhai wa watu. Siasa zinapaswa kuchukua angalau asimilia 56.7 kujenga matarajio halisi ya wananchi.