Home Makala TANZANIA ILIKUWA ‘SHAMBA LA BIBI’!

TANZANIA ILIKUWA ‘SHAMBA LA BIBI’!

2603
0
SHARE

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

Dhamira ya Rais John Magufuli katika kupigania rasilimali za watanzania kuhakikisha zinawafaidisha wote uimeibuka Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (Tahliso) ambao wanataka kasi hiyo iongezeke huku wakiipongeza.

Pia wamewaomba watanzania na wasomi kuendelea kuliombea Taifa na kumuunga mkono kiongozi huyo ambaye ana dhamira ya dhati kupeleka maendeleo yao mbele.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Stanslaus

Kadugalize anasema hakuna mtu ambaye asiyefahamu kuwa nchi ya Tanzania ilivyogeuka kuwa shamba la bili kwa kila mtu kufanya anavyotaka.

“Kwani ukiangalia kwa umakini utagundua hata baadhi ya wageni walikuwa wakituibia wanapeleka mali kwao huku wakituacha mashimo makubwa bila kunufaika na rasilimali zilizopo “Anasema

Anasema hali hiyo inatokana na baadhi ya watu waliopewa dhamana na serikali katika nyadhifa mbalimbali kukosa maadili ya uongozi kwa makusudi ama kwa bahati mbaya wamesababisha uzembe ambao umeligharimu Taifa.

Anaongeza kuwa hasara kubwa ambayo watanzania wameipata ni  kupoteza fedha nyingi ambazo zingeweza kuisaidia serikali kuboresha maisha ya watanzania katika nyanja mbalimbali za kielimu.

Mwenyekiti huyo anasema fedha hizo ambazo zimepotea zingeweza kusukuma gurudumu la maendeleo kwa kuhakikisha upatikanaji wa maji, ujenzi wa barabara, utoaji elimu bure hadi Chuo Kikuu, huduma za afya unafikiwa kwa asilimia kubwa ili kuondosha changamoto hizo.

“Fedha ambazo zimepotea leo hii zingeweza kusaidia kuinua maendeleo katika nyanja mbalimbali za kielimu, afya na kiuchumi kwa lengo la kusogeza karibu maendeleo kwa wananchi katika maeneo mbalimbali hususani maeneo ya vijijini “anasema.

Anasema juhudi kubwa zinazoonyeshwa na Rais Magufuli kupigania na kuzilinda rasilimali za nchi kwa maslahi ya Taifa ni jambo ambalo litasaidia kuchangia kwa kasi harakati za kimaendeleo.

Anaongeza tokea kiongozi huyo aingie madarakani anakaribia kutimiza miaka miwili lakini ndani ya kipindi hicho watanzania wameona mambo mengi makubwa yakifanywa na kuipa nchi maendeleo.

Anasema moja kati ya mambo makubwa ni suala la kiongozi huyo kupambana na vita dhidi ya dawa za kulevya kuondoa watumishi hewa serikalini pamoja na wenye vyeti feki .

“Lakini jambo lingine ambalo alilipigania kwa vitendo ni vita dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi sambamba na kufufua shirika la Ndege(ATC) kwa kununua ndege ambazo hivi sasa watanzania wanajivunia kuwa ni mali yao” anasema

“Licha ya hivyo lakini pia kasi yake imewezesha ujenzi wa reli ya

kisasa, ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) sanjari na utoaji wa ajira zaidi ya 50,000 kwa vijana wahitimu jambo ambalo litawawezesha kunufaika wao na jamii zao” anasema

Mwenyekiti huyo anasema Rais Magufuli pia ameimarisha utumishi wenye nidhamu na uwajibikaji serikalini kitendo ambacho kimeinua kwa kasi uchumi wa nchi kufikia wa kimataifa na kuboresha sekta ya afya ikiwemo kupunguza bei za dawa.

“Rais Magufuli ameonyesha ujasiri mkubwa kwa kuzuia mchanga wa madini ya dhahabu (Makinikia) na kuunda tume ili ichunguze namna nchi ilivyokuwa inapoteza mapato ambayo ilionyesha jinsi watu walivyoibiwa mapato ya Taifa kwa kipindi kirefu.

“Tunaona pia  hivi karibuni amekabidhiwa ripoti ya uchunguzi dhidi ya Madini ya Almasi na Tanzanite iliyochunguzwa na kamati mbili zilizoundwa na Spika Job Ndugai ripoti ambayo imeonyesha jinsi watanzania tulivyoibiwa kwa kipindi kirefu kiongozi huyo wa nchi hakusita kuwachukulia hatua waliohusika,” anasema.

Hoja hizo pia zinaungwa mkono na aliyekuwa Rais wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tanga, David Manyilizu ambaye anasema suala msimamo wa Rais Magufuli kusimamia vitu kwa umakini mkubwa utaifanya nchi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Anasema kitendo cha kiongozi huyo kuwawajibisha viongozi wasiowajibika inasaidia kuchangia kasi kubwa ya maendeleo kwa watanzania ikiwemo  kukuza uchumi kutokana na rasilimali zilizopo.

“Katika juhudi hizo za Rais Magufuli watanzania tumsaidie kwa

kumuombea kiongozi huyo aweze kufika malengo yake aliojiwekea lakini pia tunamuomba awachukulie hatua watuhumiwa wote waliohusika “ anasema.