Home Uchambuzi Tatizo si mfumo ni uongozi

Tatizo si mfumo ni uongozi

2596
0
SHARE

KUNA watu bado wanahodhi fikra kuwa tatizo la uduni wetu ni mfumo, ambao wanadhani unaweza kuzuia mabadiliko yeyote. Mimi niliwahi kuandika huko nyuma kuwa tatizo letu si mfumo bali uongozi.

Na kwa bahati nzuri zaidi, kiongozi mmoja tu katika ngazi ya Rais anaweza leta mabadiliko ikiwemo kuuondoa huu mfumo dhalimu. Tujiulize, Tanzania ya Nyerere, Kawawa na Sokoine ilikuwa ya hovyo? La hasha!

Katiba yetu (bila kujali tunavyoiponda) inatoa mamlaka kubwa sana kwa Rais kuujenga mfumo autakao. Rais John Magufuli amedhihirisha hilo kutokana na mambo aliyofanya katika kipindi kifupi tu. Na tunaamini baada ya muda ataweza kujenga mfumo thabiti wa taasisi zinazowajibika na mfumo unaolenga kulikwamua taifa kimaendeleo.

Hata hivyo napenda kutoa maangalizo mawili. Mosi, pasipo kujenga taasisi imara za kiuwajibikaji na kuandaa kada mpya ya watendaji ambao hawajachafuka (untainted) ambao watakuwa wanafunzi wa mfumo huo na watasimama kama walinzi wa kuendeleza mfumo huo, Rais Magufuli anaweza akaondoka madarakani na mfumo wake. Namshauri Rais aende mbali ya chama chake cha siasa kuangalia kada hii. Vigezo vya msingi viwe uwezo wa kuendana nna ubunifu.

Pili, katika kujenga mfumo huu kutakuwa na mambo mengi yanayoweza kutafsiriwa kama karaha, maudhi, au uonevu. Lakini hamna namna, huwezi kuujenga mfumo kwa tabasamu tu. Maamuzi magumu yanapaswa kufanyika. Na kwenye maendeleo, hatutapiga hatua bila kufunga mikanda. Lakini pia, kwa upande wa utawala wanapaswa kukubali kukosolewa. Wapokee ukosoaji na kuujibu kwa hoja ili hata huo mfumo uwe wa kidemokrasia . Tutafika.

Richard Mbunda, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam