Home Uchambuzi Uzalendo wetu upo wapi?

Uzalendo wetu upo wapi?

2746
0
SHARE

MOJAWAPO ya vitu ambavyo Watanzania wanakosa ni uzalendo. Ni ngumu kujua chanzo lakini nadhani ni kwa vile tumeshindwa kuwa na utambulisho baada ya kudhani kuwa vita dhidi ya ukabila pia ilimaanisha tutupie mbali tamaduni na asili zetu mbali mbali ambazo kwa ujumla wao ndio zingejenga taswira ya taifa.

Leo hii wengi wetu hatujivunii asili zetu na matokeo yake hili linakwenda hadi juu kwenye ngazi ya taifa ambapo ni rahisi kwa mtanzania kujiunga na wageni kutukana na hata kukejeli nchi yak.

Cha ajabu pale ambapo hao wageni wanaisifu nchi yake yeye hukataa kukubali na kuanza kusema kuwa sio sifa za kweli na zilikuwa na lengo la kutufanya tubweteke na kujisahau!

Sasa najiuliza mbona wakikosoa na hata kukejeli nchi yetu wengi wetu hukubaliana nao na kuwaunga mkono pasi na shaka wala kusitasita? Uzalendo wetu upo wapi?

Maana ya uzalendo haimaanishi kuwa msafi lakini ni kuudhihirishia ulimwengu kwamba unajivunia nchi yako hata kama yapo mapungufu fulani fulani, mengi mazuri pia yapo.

Nimepata bahati ya kusafiri nje ya nchi sehemu mbali mbali duniani na kila utakapowakuta watanzania, tabia na alama ya kwanza ni kwa wao kujifanya kuwa ni wenyeji sana huko majuu na hujitahidi kuzungumza lugha za hao wageni na hata ku-act kama hao wageni.

Pindi wakijua kuwa umetoka Tanzania na ukawasalimia kwa Kiswahili, ghafla wataendelea na kuchangamana na wageni na mara nyingi wanaweza hata kukupuuzia huku wakikonesha mbwemwe kuwa wao kule ni wenyeji na wewe ni wakuja tu!

Cha ajabu jirani zetu hapa Afrka Mashariki ambao tunawatuhumu kuwa na ukabila wakikutana huko nje huwa wamoja na wenye kupenda kusaidiana bila kujali tofauti zao za ukabila ambazo huziendekeza wakiwa nyumbani.

Cha ajabu Mtanzania ndiye atakayewakimbia wenzake na huku akijifanya yeye ni wa kule sana kuliko huku nyumbani! Sijui nini kifanyike kubadili hali hii?

Emmanuel Kihaule, Dar es salaam