Home Makala WANASIASA WANAVYOCHOCHEA KUANGUKA KWA UCHUMI WA AFRIKA

WANASIASA WANAVYOCHOCHEA KUANGUKA KWA UCHUMI WA AFRIKA

1713
0
SHARE

NA FARAJA MASINDE,

NI miongo kadhaa sasa imepita tangu kushika kasi kwa siasa za barani Afrika kwa Viongozi mbalimbali kupata mwanga wa kujipambanua kihoja na kimikakati lengo likiwa ni katka kutimiza azima zao za kuwatumikia wananchi.

Hata hivyo kwa nyakati tofauti kila mtu amekuwa na mtazamo wake juu ya kile kinachofanywa na wanasiasa wa Afrika kwa nyakati tofauti pindi wanapopewa nafasi ya kuwa wawakilishi wa wananchi.

Kwani tumeshuhudia kwenye mataifa mbalimbali ‘Wanasiasa’ wakiwa ni chanzo cha migogoro ambayo imekuwa ikipelekea kuvunjika kwa mani kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Mataifa kama Kongo DRC, Sudani, Gambia, Burundi, Afrika ya Kati, Afrika Kusini na kwingineko yakiingia kwenye machafuko kwa sababu tu za kisiasa jambo ambalo limefanya wananchi wengi kuyumia muda wao mwingi kwenye machafuko kuliko kufanya shughuli za kujiletea maendeleo.

Pia mbali na hilo kumekuwapo na sura nyingine ambayo imekuwa ikitumiwa na baadhi ya viongozi hawa wa Afrika kujicheleweshea maendeleo yao wao wenyewe kwa kuruhusu maslahi yao binafasi.

Hii inatokana haswa na kubariki kusainiwa kwa mikataba mibovu ambayo mwisho wake imekuwa na matokeo hasi kwenye kusukuma maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Na ninapolizumngumzia hili Tanzania imwekuwa ni miopngoni mwa nchi hizi ambazo baadhi ya viongozi wake wamekuwa mstari wa mbele kuhujumu uchumi wa mataifa yao bila ya kujali kundi kubwa liloko nyuma yao.

Pamaoja na kwamba Bara la Afrika limekuwa likiongoza kwa kuwa na raslimali nyingi zenye utajiri mkubwa unaoweza kugeuza maish ya watu wake na maenedeleo kwa ujumla lakini gviongozi wake wamesalia kuyajali matumbo yao zaidi kwa kuzitumia raslimali hizo kinyemela.

Hali hii ndiyo inayotafsriwa kama chanzo cha Afrika kuwa omba omba kwenye mataifa ya kigeni licha ya kuwa na raslimali za kutosha kama dhahabu, gesi na hata mafuta kutokana tu na baadhi ya viongozi wake wakuingia mikataba inayowanufaisha wao wenyewe kwa muda ambao wanakuwa madarakani.

Hali inaonyesha kuwa kundi kubwa la wanasiasa wanaojitumbukiza kwenye ulingo huo kila mmoja amekuwa na malengo yake wakiwamo wale wanaojitenga mbali na utumishi wa Umma, kwakuwa wengi wana malengo ya kushika nyadhifa na ama vyeo kujinufaisha.

Hivyo kwa mantiki hiyo hawawezi kujitathimini hasa wakiwa madarakani.

Tumeshuhudia mijadala na makongamano mbalimbali ambayo yamekuwa yakiandaliwa na taasisi mbalimbali kwaajili tu ya kutoa mwanga na tathimini kwa viongozi wa afrika lakini yanaokana bado hayana tija kufuatia wengi kutotilia maanani misingi hiyo.

Kwa namna hali ilivyo Afrika ni viongozi wasiokuwawanasiasa tu ndio wanaoweza kukabiliana na udhorotaji wa maendeleo ambao umekuwa ukisababishwa na baadhi ya wanasiasa wanaochumia matumbo yao.

Inasikitisha kuona kuwa wanasiasa hawa wamekosa kabisa utu dhidi ya watu wanaowawakilisha na ambao ni kundi kubwa liloko nyuma yao na badala yake wameweka mbele ma maslahi yao binafsi nakushindwa kuwaletea wananchi maendeleo.

Hata watumishi wa serikali ambao wameaminiwa na kupewa nafasi mbalimbali za kufanya maamuzi kwa faida ya wengi au taifa nao kwa miaka ya hivi karibuni wamejikuta wakifunikwa na  mwamvuli huu wa udanganyifu huku wakipatiwa nguvu kubwa na wanasiasa.

Hivyo hata watumishi hao wa serikali licha tu kwamba wamekuwa wakila kiapo lakini wamepoteza kabisa uaminifu na hivyo kujimkuta wakiyagharimu mataifa yao hali inayofanya kuibaki nyuma kimaendeleo kwa tama zao tu za kuingia mikataba tata.

Tumeshuhudia namna ambavyo wanasiasa wamesiama katikati katika kuwatetea na kuwalinda wakwepaji kodi ya mapato, wapitishaji mikataba tata, wawekezaji hewa, upotevu wa mapato udanganyifu wa mali zinazosafirishwa nje ya nchi na mambo mengine yenye sura kama hiyo.

Kuwa na viongozi ambao hawafungamani na siasa tumeshuhudia namna ambavyo wamejikita zaidi katika kusimami kile wanachokiamini kwenye utendaji wao bila kusubiri kuambiwa wala kulishwa maneno.

Hili linaweza kuthibitishwa na Rais Dk. John Magufuli ambaye tangu kuingia kwake madarakani Novemba 5 mwaka juzi tumeshuhudia namna ambavyo walivyoweka siasa pembeni na kujikita zaidi katika kupigania maendeleo ya wananchi wake na taifa lake kwa ujumla.

Kiongozi huyu amekuwa ni kati ya viongozi wachache ambao wanaamini kuwa Afrika ina raslimali nyingi ambazo kwa mantiki hiyo kamwe haipaswi kuwa omba omba kwenye matifa ya kigeni ambayo nayo yamekuwa yakivuna utajiri wao kupitia raslimali za Afrika.

Pamoja na kwamba wengi walikuwa wakimbeza kiongozi wa namna hii ambaye siyo mwanasiasa lakini ni dhahiri kuwa kwasasa wanamwelewa kwa kile anachoendelea kukifanya kwani amekuwa akikifanya kwa dhati ya moyo wake.

Ni Mtanzania wa ajabu tu ambaye hadi leo hii bado hajaelewa wala kutambua dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo na kufuta umasikini iliyobebwa na kiongozi huyu wa ajabu kuwahi kutokea.

Kwani kwa kipindi kifupi ameweza kutufunulia tambala lilokuwa limeficha wahujumu uchumi wa ndani na nje ya nchi, kama hiyo haitoshi ameweza kutuonyesha namna ambavyo wasiokuwa watumishi walivyofanikiwa kuneemeka na mishahara ambayo hawaitolei jasho.

Na kama hiyo haitoshi bado ameweza kutuonyesha namna ambavyo makampuni ya kigeni kwa kushirikia na baadhi ya wanasiasa na watendaji wa serikali wasiokuwa waaminifu namna ambavyo walikuwa wakinufaika na madini yetu kwa miaka mingi.

Takribani trilioni 230 zuimepotea kwa kipindi chote kiwango ambacho kingeweza kabisa kuendesha nchi hii kwa miaka mitatu flulizo.

Kitu kinachoumiza ni kwamba waliohusika wapo na bado walikuwa wakiendelea kupokea fungu lao ili hali amendeleo ya nchi kwa ujumla yakisalia kuwa pale pale, hili ni jambo linaloumiza sana.

Wanasiasa wetu kwa kiwango kikubwa wamehusika moja kwa moja katika kuuudidimiza uchumi wa Afrika kwa manufaa yao bila kujari kundi kubwa lililoko nyuma yao.

Kwani tayari tumeoneshwa uhalisia wa hili kupitia kwa Rais Magufuli ambaye pasi na shaka yoyote kuwa kiongozi huyu anafaa kuwa kielelezo cha Afrika mpya.

Na tayari tumeshuhudia namna ambavyo viongozi mbalimbali wan chi za afrika wakionyesha kuvutiwa na utendaji kazi wake na hata wengine kwenda mbali zaidi kwa kutamani kusafiri hadi Tanzania kwaajili ya kuja kupata mbinu za namna ya kukabiliana na wahujumu uchumi wa mataifa yao.

Hatuna budi kuendelea kumuombea kiongozi huyu ile tumeweze kuvuna mengi zaidi yaliyo na tija kwa taifa leo ambayo tumaani kuwa yatatuletea maendeleo barani Afrika.

Huu ni wakati wa kuweka itikadi zetu za vyama pembeni na kushikamana bega kwa bega kwaajili ya kuufufua uchumi wetu ili kuweza kuondokana na umasikini ambao umedumu na si kwa zaidi ya miaka 50 sasa.

Tumekuwa na baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakiongea ukweli juu ya uchungu wa raslimali zetu lakini ama kwa kujua au kwa kutokujua wamekuwa wakikosa nafasi ikiwamo kupuuuzwa kwa madai ya kuingilia mambo ambayo ni siri na mfumo huu ni wazi kuwa unaonekana ndio unayoyatafuna mataifa mengi ya Afrika kwa kiwango kikubwa.

Hivyo umasikini wetu ulikuwa ukisababishwa na wanasiasa wenyewe ambao ndiyo wametufikisha hapa japo licha ya ukweli huo lakini bado  nao wamekuwa wakikanusha vikali.

Naamini kwa mwendo huu wa viongozi wasiokuwa wanasiasa tutaendelea kushuhudia mengi ambayo yalikuwa yamefichwa kwenye mgongo wa siasa na usiri mkubwa.

Viongozi aina ya, Rais Magufuli ndoo wanaohutajika kwasasa barani Afrika kwaajili ya kujenga uchumi mpya ambao umenguka kwa tama za viongozi wasiokuwa waadilifu.